MAJINA 6 YA WATAKAOWANIA NAFSI YA UBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARI KIPITIA CHADEMA
Kamati
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewateua washiriki sita
kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala).
Katika
kikao kilichofanyika jana mjini Zanzibar walioteuliwa ni Profesa Abdalla
Safari, Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha na
Pamela Massay.
Taarifa
ya leo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema,
Tumaini Makene imesema wateule hao watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa
mujibu wa utaratibu, Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.
Masha
na Wenje, walishiriki uchaguzi uliofanyika Aprili 4 ambao Chadema ilipeleka
majina yao pekee jambo lililozua mjadala bungeni na kuhitimishwa kwa wao kupigiwa
kura za Hapana.
Katika
uchaguzi huo, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba
wa Eala.
Kwa
upande wa CCM, walioshinda ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya,
Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Adam Kimbisa na kutoka CUF iliyokuwa
na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa
akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo.
No comments