VIDEO: MAALIM SEIF AFUNGUKA MAMBO MAZITO KUHUSU MGOGORO WA CUF
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchini ndiye anayejaribu kupandikiza mgogoro ndani ya chama
hicho kwa maslahi yake binafsi.
Ameyasema
hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha 360 kinachorushwa
na CloudsTv. kilichopo Jijini Dar es salaam.
Amesema
kuwa hakuna haja ya wanachama kuwa na hofu kuwa chama hicho kinaweza
kusambaratika hivyo amewataka kuimarisha mshikamano uliopo ndani ya chama
hicho.
“Nachojua
mimi hakuna mgogoro ndani ya CUF kama inavyoelezwa na baadhi ya watu, isipokuwa
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini anajaribu kupandikiza mgogoro huo kwa maslahi
yake binafsi,”amesema Seif.
Aidha,
ameongeza kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanatumiwa kutaka kukivuruga chama
hicho, hivyo amesema kamwe hawatafanikiwa.
Hata
hivyo, amesema yeye kama kiongozi ataendelea kufanya shughuli zake za chama na
kuwataka walio chini yake wasivunjike moyo.
No comments