MCHUNGAJI ANAYEDAIWA KUUAWA AKUTWA HAI AKIBATIZA WATU KANISANI
Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Usharika wa Mbinga, Leonard Kambo ambaye alidaiwa kuuawa na watu
watano wa kanisa hilo amekutwa akitoa ubatizo katika usharika wa KKKT Kitandilo,
Makambako, Mkoani Njombe.
Wakati
Mchungaji huyo aliyedaiwa kuuawa mwaka 2011 akionekana akitoa ubatizo kanisani,
watu waliodaiwa kumuua mchungaji huyo wamo mahabusu tangu mwaka huo 2011.
Ndugu
wa watuhumiwa wa mauaji hayo ndio waliohaha kusaka picha ya mchungaji huyo
baada ya kupata taarifa kwamba alihamishiwa eneo la Makambako baada ya kutokea
tuhuma kwamba ameuawa.
Kwa
mujibu wa habari hizo, baada ya ndugu kupata taarifa kwamba mchungaji huyo yupo
hai, walitumia kila njia kupata picha yake ili itumike kama ushahidi kwamba
yupo hai na tuhuma dhidi ya wauaji si za kweli.
Muumini
mmoja wa kanisa hilo alieleza kuwa ndugu wa watuhumiwa hao walihakikisha
wanamnasa mchungaji huyo kwa kamera popote alipo ili wasitishe kifungo cha
ndugu zao na uongo dhidi yao.
Mmoja
wa watuhumiwa wa kesi hiyo ambaye alikamatwa kisha kuachiliwa huru, Leonard
Myale alisema kuwa baada ya kumuona na kupata picha ya mchungaji huyo akiwa
hai, watathibitisha Polisi ili akamatwe na watuhumiwa wengine waachiwe huru.
“Tumeteswa
sana, tumedhalilishwa, tumepuuzwa na kusemwa vibaya na Wakristo wenzetu, ndugu
zetu na hata jamii haikutuamini juu ya tuhuma hizi za uongo ambazo hata Polisi
walitubambikiza kesi bila kufanya utafiti wa kina. Tulikanusha kuhusika na
mauaji hayo lakini Polisi hawakutuamini. Sasa tunaamini tuko huru, wenye
mamlaka watachukua hatua za kutusaidia” alisema Elenia Mhoka mtuhumiwa mwingine
wa mauaji hayo.
Aidha
aliyewahi kuwa Mchungaji wa KKKT Kitandililo, Geofrey Mtweve, alitafutwa ili
kueleza kuhusiana na suala hilo, lakini hakutaka kuzungumza chochote na kusema
kuwa yeye siyo msemaji wa kanisa hilo.
“Mimi
si msemaji wa kanisa ila ni kweli nilikuwa Kitandililo, uongozi umenihamisha
kuja Ilembula, nimebadilishana na Mchungaji Leonard Kambo, ambaye ndiye
nimemkabidhi usharika, mengine sifahamu lolote. Wasiliana na uongozi wa Jimbo,”
alisema Mtweve.
Aidha
mchungaji Kambo alipotafutwa na kuulizwa kuhusiana na yeye kutuhumiwa kifo na
kama ni kweli aeleze kuwa alifufuka lini, lakini mawasiliano yakawa mabovu.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, baada ya kuelezwa tukio hilo aliomba kupatiwa
picha na namba ya RB na kuahidi kuwa atalifanyia kazi suala hilo.
Credit:
TanzaniaDaima
No comments