UHAMIAJI YAANZA KUHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI.
Idara
ya uhamiaji leo imezindua huduma ya
mfumo wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki.
Amesema hayo jijini Dar es salaam kamishna
jenerali wa uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala
kuwa lengo la kuzindua mfumo huo ni kuimarisha udhibiti wa wageni
waishio hapa nchini pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya serikali.
Ameongeza
kuwa mfumo unatoa fursa kwa waajiri na wageni wote wenye vibali vya ukaazi
kuhakiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na mamlaka husika.
Dkt.Makakala
amezitaka taasisi na mashirika baada ya kuhakiki vibali vya wageni wao kupitia
mfumo huo kuwasilisha taarifa za vibali hivyo katika ofisi ya za uhamiaji za
mikoa katika maeneo yao endapo watabaini matatizo.
Idara
ya uhamiaji imetoa muda wa siku tisini tangu kuzinduliwa mfumo huo ili kuhakiki
taarifa za vibali vya wageni na kusema ambao watakuwa hawajahakiki vibali
hatua za kisheria zitachukuliwa.
Idara
imetoa wito kwa waajiri na wamiliki wa makampuni na wote wenye vibali vya
ukaazi kutoa ushirikiano katika kipindi chote.
No comments