TBL YAZINDUA KAMPENI YA ‘CASTLE LITE UNLOCKS’ JIJINI DAR
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Idara ya
Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni
ijulikanayo, ‘Castle Lite Unlocks’. Kushoto ni Meneja Chapa Msaidizi wa Bia
Laini Tanzania, Isaria Kilewo na katikati ni Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha
Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.
Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha Bia Laini
Afrika Mashariki, Amou Majok (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakibadilishana mawazo katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
KAMPUNI
ya kutengeneza Bia Tanzania (TBL)) leo imezindua kampeni ijulikanayo, ‘Castle
Lite Unlocks’ ambayo lengo lake ni kuhamasisha wateja wake wa bia chapa Castle
Lite kuifurahia zaidi na pia kuwaleta pamoja katika tamasha kubwa litalofanyika
mwezi wa Julai mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
uliofanyika katika ofisi za TBL zilizoko Masaki, Meneja Masoko wa TBL Idara ya
Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe, alisema TBL kwa miaka
imekuwa ikijikita katika kuwafurahisha na kuwachangamsha wateja wake, hasa
vijana kwa matamasha ikiwemo muziki ambao upo katika vipaumbele vya kampuni
hiyo.
“Uzinduzi huu utafikia kilele chake tarehe 22
mwezi wa Julai mwaka huu ambapo kutakuwa na tamasha kubwa Dar es Salaam
litakalowapa nafasi wateja wetu kushuhudia wanamuziki wakubwa wa ndani na nje
ya nchi, hivyo kuwapa wateja burudani itakayokuwa kwenye kumbukumbu zao kwa
muda mrefu”, alisema Kavishe.
Kavishe aliongeza kuwa kwa kipindi hicho cha
miezi mitatu ya kampeni, zawadi kedekede zitatolewa zikiwemo muda wa maongezi
wa simu za mkononi wa zaidi ya milioni 30 na pia tiketi zaidi ya elfu moja kwa
washindi wa droo ambazo zitakuwa zinashindanishwa.
Aliongeza kwamba bajeti ya kampeni nzima ni zaidi
ya shilingi milioni mia saba.
Naye Meneja Masoko wa TBL Kitengo cha Bia Laini
Afrika Mashariki, Amou Majok alisema kuwa TBL ina utaratibu mahsusi wa kuandaa
matamasha mara kwa mara ili kuwashukuru wateja wake kwa kuwapa burudani na kuwahamasisha
kuzifurahia vinywaji vyake ambavyo ni vya hali ya juu na vyenye ubora
zaidi.
No comments