NAPE: NIKISEMA UKWELI NAONEKANA MKOROFI, MENGINE NIMEYASHUHUDIA MWENYEWE
Mbunge wa jimbo la
Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa ya
moyoni kwa kusema kila anapokumbuka shida wanazozipata wananchi humfanya
aonekane mkorofi kwa kuwa anasema ukweli.
Nape amebainisha
hayo, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter huku akiwa ameambatanisha na
picha ambayo inaonesha wananchi jinsi wanavyopata tabu kuvuka upande mmoja wa
mto kwenda upande wa pili kwa kupita ndani ya maji hayo.
“Niliyashuhudia maisha haya mikoani kwa miezi 38, nadhani ndiyo
nikiyakumbuka naonekana mkorofi !! iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele
vyetu”. Ameandika Nape
Niliyashuhudia maisha haya mikoani(38months),nadhani ndio nikiyakumbuka naonekana mkorofi!!Iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu!
12:00 AM - 17 Apr 2017
No comments