MAREKANI: HAKUNA MUDA WA ZIADA WA KUVUMILIA VITISHO VYA KOREA KASKAZINI
Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert
Raymond McMaster amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu
dhidi ya Korea Kaskazini inayoendelea na vitisho vya silaha za Nyuklia.
McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya
vitisho vya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China.
Amesema kuwa kuna makubaliano ya kimataifa, ikiwemo China
kuhakikisha tabia hii haiendelei, kwani kumekuwa na majaribio ya makombora ya
hivi karibuni yanayoonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini hali ambayo
hawataivumilia zaidi.
Amesema kuwa Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika
wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.
Korea Kaskazini imefanya jaribio la uzinduzi wa makombora ya
masafa ya mbali, hata hivyo lilikwama, ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Mike
Pence amefika Korea Kusini saa chache baada ya jaribio hilo.
Akizungumza katika kambi ya jeshi, Pence amesema anawahakikishia
kuwa chini ya uongozi wa Rais Trump ushirika wa Marekani Korea
Kusini haujawahi kuwa na nguvu lakini kwa msaada wa jeshi hilo na Mungu uhuru
utaendelea kuimarika katika rasi ya Korea bila vitisho vyovyote
No comments