MAZOMBIE YENYE SILAHA YAVAMIA MKUTANO CUF YA MAALIM SEIF, WANANCHI WAFANIKIWA KUMDHITI MMOJA
Watu wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande
unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo,
ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia
soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na
waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo.
Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF
ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.
Mtu huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na
wenzake katika eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi
huo katika mkutano wa wanachama wa CUF.
Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.
Pichani
mmoja kati ya watu wanaotuhumiwa kuvamia mkutano huo mara baada ya kudhibitiwa
na wananchi wenye hasira akijaribu kikimbia mara baada ya kufanya uvamizi huo
No comments