KOREA KASKAZINI YATOA VITISHO VINGINE KWA MAREKANI
Wakati kukiwa na
taharuki kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusu matumizi na majaribio ya
mabomu ya nyuklia yanayofanywa na nchi hiyo ya bara la Asia, imetoa msisitizo
wa vitisho vingine.
Makamu Waziri wa
Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Han Song-ryol ameiambia BBC kuwa nchi hiyo
haiogopi vitisho vya Marekani na kwamba wamejipanga kufanya majaribio ya
makombora yake kwa mfumo wa kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.
Alisisitiza kuwa
vita kamili ya nchi hiyo itakuwa ni matokeo ya Marekani kuchukua hatua zozote
za kijeshi dhidi yake.
“Kama Marekani inapanga mashambulizi
ya kijeshi dhidi yetu, tutajibu kwa makombora ya nyuklia kwa namna yetu na njia
yetu wenyewe,”Han anakaririwa na
BBC.
Kauli hiyo imekuja
ikiwa ni siku chache tangu Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence kuionya Korea
Kaskazini kuwa muda wa kuivumilia umekwisha na kuwataka waache kuijaribu
Marekani.
Pence alisema kuwa
Korea Kaskazini haipaswi kumjaribu Rais Donald Trump akiwataka kuona mfano wa
kipigo alichowashushia Syria na Afghanistan hivi karibuni.
Korea Kaskazini
imeendelea na mpango wake wa kuandaa na kufanya majaribio ya mabomu ya nyuklia
ingawa hatua hizo zimekuwa zikilaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa.
Nchi hiyo imelenga
katika kuhakikisha inatengeneza makombora yanayoweza kufika katika pande kadhaa
za dunia ikiwa ni pamoja na Marekani.
Rais wa Marekani,
Donald Trump amesema kuwa mpango huo hautawezekana na tayari ameanza kutuma
vikosi vya
No comments