Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na
filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia wakionesha cd
hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la
Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)
Muuza CD za Tamthilia
na Filamu za nje,Marick Omary,akizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa
Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba serikali
kuwasaidia na kutowafungia vijana hao kuuza cd hizo kwa kuwa zinawapatia
ridhiki ya kihalali tofauti na kufanya kazi zingine zisizo za kihalali.
Muuza CD za Tamthilia
na Filamu za nje,Andhuhuri Mohamedy,akichangia hoja kwa waandishi wa habari
katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuiomba
serikali kuwaruhusu wafanyabiashara hao (Machinga) kuendelea na biashara hizo
ambayo inawawezesha kulisha na kusaidia familia zao na kusema kama kuna maboresho
ni bora serikali wakae kwa pamoja wazungumze siyo kupiga marufuku watakufa
njaa.
Muuza CD za Tamthilia na Filamu za nje,Halima
Bakari,akizungumza kwa majonzi kuhusu kuiomba serikali kuweka utaratibu mzuri
wa kuwaruhusu wafanyabiashara hao waendelee na uuzaji wa tamthilia na filamu za
nje kuendelea kuuza kwa kuwa kuna wanawake wengi wameachana na suala la kuuza
miili yao (Biashara ya Ngono) ambayo siyo halali wakajiingiza kuuza cd hizo ili
wapate kipato cha kihalali kwa hiyo kuwafungia ni kuwarudisha nyuma kifikra.
Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika
eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
Vijana ambao ni machinga wanaouza CD za Tamthilia na
filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia wakionesha cd
hizo juu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtaa wa Aggrey eneo la
Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
|
Baadhi ya wauzaji wa CD hizo waliokusanyika katika
eneo hilo la Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo
|
|
Baadhi ya maduka yaliyokuwa yakiuza CD za Tamthilia
na filamu za kizungu,Kihindi na za kutoka bara la asia yakiwa yamefungwa kama
yanavyoonekana katika Mtaa wa Aggrey eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
NA ELISA SHUNDA, DAR
WAFANYABIASHARA
wadogo wadogo ‘Machinga’ wanaouza filamu za kigeni wameandamana wakiomba
kukutana na Rais John Magufuli ili kusikilizwa juu ya kupigwa marufuku kuuza
filamu hizo hapa nchini.
Marufuku hiyo
ilitolewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe,
siku chache baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo mara baada ya kukutana na
waigizaji wa ndani ambapo walieleza malalamiko yao juu ya filamu za nje
kuharibu soko la kazi zao.
Wamachinga hao
waliandamana jijini Dar es Salaam jana katika soko la Kariakoo katika Mtaa wa
Aggrey ambako kuna maduka
wanakoenda kuchukua mikanda ya filamu za nje ‘CD’ na kusambaza mtaani huku
wengine wakiweka katika vibanda kwa ajili ya kukodishia wateja wanaohitaji.
Wakizungumza na
waandishi wa habari wafanyabiashara hao walisema Waziri huyo alitoa maamuzi hayo
kwa kusikiliza upande mmoja ambao ni walalamikaji bila kuwapa nafasi ya
kujieleza jambo ambalo wanalipinga.
Mmoja wa machinga
hao Hanzuruni Mohamed alisema aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo Nape Nnauye
alikuwa akisikiliza pande zote kabla kufanya maamuzi na kuongeza kwamba
walishakaa vikao mbalimbali kwa ajili kutafuta mwafaka lakini Mwakyembe
ameshindwa kufanya hivyo.
“Nape alikuwa
anafanya maamuzi kwa kufuata pande zote mbili, huyu katoa siku 10 tu kufungia
filamu za nje, hapa kuna vijana zaidi 1000 fikiria tutafanya kazi gani, tukiwa
panya road nchi itakuwaje tunakuomba Rais uliangalie hili sisi ni vijana wako”
alisema Mohamed.
Naye Halima Bakari
alisema kufungwa kwa biashara hiyo kutamwathiri maisha yake kwani alikuwa
akitegemea biashara ya filamu kuendesha maisha yake na kuhudumia familia yake
na kusema awali alikuwa akifanya biashara ya kujiuza biashara aliyoiacha baada
ya kujiingiza katika soko la filamu.
“Mwanzo nilikuwa
najiuza nategemewa na mdogo wangu yatima, sasa hivi mabosi wamefunga maduka
wakisema wanaogopa kufungwa kutokana na kauli ya Waziri, sasa hivi hatuna ajira
nyingine mimi ni binti bila kutoa penzi sipati kazi na kauli mbiu ni Hapa kazi
tu, Rais tusaidie tutaenda wapi” alisema Bakari.
Kwa uapnde wake
Maliky Ally alisema wametii kuacha kuuza filamu lakini wamaomba kusikilizwa
upya ili kuwe na makubaliano yatakayohusisha pande zote kwasababu hiyo ni ajira
wanaoitegemea kuendesha maisha yao.
|
No comments