JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LIMELAANI KUSHAMBULIWA WAANDISHI WA HABARI WALIOKUWA WAKITEKELEZA WAJIBU WAO KITAALUMA.
Jukwaa
la wahariri Tanzania (TEF) limelaani tukio la kushambuliwa na kuumizwa waandishi wa habari waliokuwa wakitekeleza
wajibu wao kitaaluma.
Aidha
TEF limetoa wito kwa jeshi la polisi kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo na
kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote waliohusika na kuujulisha umma wa
watanzania kutambua kuwa waandishi wa habari wanatekeleza majukumu yao kwa
mujibu wa sheria.
Akisoma
Tamko hilo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Bw.THEOPHIL MAKUNGA jijini
DAR ES SALAAM wakati akizungumzia kitendo cha kujeruhiwa waandishi hao
waliokuwa kazini.
Alisema
waandishi wa habari walikuwa katika mkutano wa kihabari na kusema kuwa licha ya
mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha cuf
vyombo vya habari vimekuwa vikitoa fursa ya kuandikwa na kutangazwa kwa
habari za pande zote mbili zinazovutana.
Bw.
MAKUNGA Alibainisha kuwa jukwaa hilo limefanya ufuatiliaji na mawasiliano na
pande zote mbili yaani upande wa katibu
mkuu maalim SEIF SHARIF HAMAD na ule wa mwenyekiti anayetambuliwa na msajili wa
vyama Pofesa IBRAHIM LIPUMBA na kubaini kuwepo kwa viashiria vya mashambulizi dhidi ya waandishi kutoka
kwa watu au kundi linalomuunga mkono Profesa.LIPUMBA.
Alisema
TEF lilifanya mawasiliano na mwenyekiti Prof LIPUMBA tarehe 24 April kwa lengo la kupata kauli
yake kuhusu kilichotokea lakini hadi
sasa hajatoa kauli yoyote tofauti na katibu mkuu maalim SEIF ambaye ametoa pole
na kulaani kitendo hicho.
Mapema
wakitoa ushuhuda jinsi tukio hilo lilivyotokea waandishi wa habari waliokutwa
na shambulio hilo wamelaani vikali kitendo hicho na kuiomba serikali na vyombo
vya dola kufanya uchunguzi haraka na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika kwani
tukio hilo sio la kufumbiwa macho ni jambo ambalo limewasababisha hofu kubwa wao
kama waandishi wa habari.
Waandishi
wa vyombo vya habari walikutwa na shambulio hilo ni kutoka chanel ten, mtanzania,
nipashe, uhuru, mwananchi ,clouds media na the guardian.
No comments