MAREKANI YAANZA KUJENGA MTAMBO KUZUIA MAKOMBORA YA KOREA KASKAZINI
Korea
Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa
kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.
Mtambo
huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa
Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio
kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.
Wizara
ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari
kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kumekuwepo
na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo
panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.
Mtambo
huo unajengwa katika wilaya ya Seongju
China
imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.
Rais
wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua
kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa
Korea Kaskazini.
THAAD
ni nini?
Ni
teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani
ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
Hugonga
kombora la kuliharibu
Ina
uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita
150 angani
Marekani
imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa
mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Chanzo:
BBC
No comments