WAZIRI MWAKYEMBE AELEZA ALIVYOZIDIWA KETE NA AGNES (MASOGANGE) SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA, AMTAJA KIJANA WAKE AMBAYE YUKO HATARINI KUUAWA GEREZANI
Waziri
wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe ameendelea kufunguka jinsi
alivyokwama kudhibiti upitishwaji wa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa
Dar es Salaam wakati alipokuwa Waziri wa Uchukuzi hadi kuzidiwa kete na Agnes
Masogange
Waziri
Mwakyembe akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast amesimulia
kilichotokea wakati alipotaka kumdhibiti binti mmoja aliyedaiwa kupitisha
masanduku matano ya 'materials' za kutengenezea dawa za kulevya aliyekamatwa
nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania.
Amesema
baada ya kufuatilia sakata lile mbali na kuchukua hatua kwa watu waliomsaidia
kupitisha mzigo uwanja wa ndege, aliamua kufanya jitihada za kumkamata binti
huyo ili achukuliwe hatua, lakini muda mfupi baada ya binti huyo kurejea
nchini, yeye alihamishwa wizara, hivyo kukosa nguvu ya kumshughulikia, hatua
iliyofanya binti huyo kumfanyia "nyodo".
Kumbukumbu
zinaonesha kuwa binti ambaye alikamatwa nchini Afrika Kusini wakati huo kwa
madai hayo, na kisha Waziri Mwakyembe kumfuatilia hadi kutimua baadhi ya
watumishi wa uwanja huo Mwezi Agost mwaka 2013 alikuwa ni 'video queen' maarufu
nchini, Agnes Gerald 'Masogange'.
Vilevile
Mwakyembe amesema kijana wake mmoja anayefahamika kwa jina la Jingu ambaye yuko
gerezani, anapaswa kuongezewa ulinzi kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa jemedari wa
kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, lakini baadaye aliundiwa kesi na sasa
huko gerezani anakutana na watu ambao wanaweza kumdhuru kutokana na kwamba yeye
ndiye aliyesababisha wafungwe.
No comments