SAFARI YA KWANZA YA TRENI MCHONGOKO KUANZA RASMI LEO
Safari ya kwanza ya treni ya kisasa ya Mchongoko (Electric Multiple Unit - EMU ) kuanza leo Novemba 1, 2024 kuanzia Stesheni ya Magufuli jijini Dar es Salaam hadi Stesheni Kuu ya Samia jijini Dodoma.
Treni hiyo Mchongoko (Electric Multiple Unit - EMU) ambayo itakuwa na vichwa mbele na nyuma tofauti na treni za awali zenye kichwa kimoja, itakuwa na uwezo wa kubeba jumla ya abiria 589 na inatembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa.
No comments