MAMIA WAJITOKEZA KAMBI MADAKTARI BINGWA
Msimamizi wa kituo cha Afya Mart, Dokta Mbishi Matumbo akifafanua jambo katika ufunguzi wa zoezi la kutoa huduma za afya mapema leo Novemba 1, 2024 makao makuu ya kituo hicho buguruni jijini Da es salaam.
Mkazi wa Buguruni Mivinjeni, Bi. Suzy Shabani akizungumza mara baada ya kupata huduma za vipimo kutoka kwa mapema leo Novemba 1, 2024 makao makuu ya kituo hicho buguruni jijini Da es salaam.
Na Neema Mpaka, Wananchi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani wametakiwa kuiitokeza kwa wingi kupata huduma za matibabu ya kibingwa na vipimo kwa siku mbili katika kituo cha Dokta Margareth Nyambo kilichopo Buguruni 'Maarufu Mart' jijini hapa.
Akizungumza kwa niaba ya Jopo la madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali nchini, ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambao wamepiga kambi hospital hapo ikiwa ni mwendelezo wa utoaji huduma kwa wiki ya mteja.
Akizungumza mapema leo Novemba 1, 2024, Msimamizi wa kituo hicho Dkt. Mbishi Matumbo amesema lengo la zoezi hilo ni kuimarisha afya ya jamii kwa kuwafikia watu wengi zaidi.
"Kama mnavyoona hapa kuna madaktari bingwa wa mama na watoto, pia kuna huduma za maabara na vipimo kwa magonjwa ya Sukari, Presha, magonjwa mengine ya watoto na wanawake". Alisema Dkt. Matumbo na kuongeza kuwa
"Nitoe wito kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi ili kupima afya zao sanjari na kupata tiba stahiki, kwa kuzingatia afya ndio maendeleo yenyewe kwa mtu binafsi na taifa kwa jumla".
Nae Mkazi wa Buguruni Mivinjeni, Bi. Suzy Shabani akizungumza mara baada ya kupatiwa huduma kituoni hapo amepongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa madaktari hao bingwa huku wakishauri serikali kuangalia namna ya kuwezesha upatikanaji wa kambi za kutoa huduma za kibingwa mara kwa mara sababu zinapunguza ukubwa wa gharama za matibabu.
"Tunamuomba Rais Dkt. Samia atusaidie sana wanawake kwenye kupunguza gharama za magonjwa ya uzazi. Ukweli wengi tuna changamoto hii lakini hatuna fedha, na matokeo yake tunafika hospitali kwa kuchelewa, na mwisho wengi hupoteza maisha," Alisema Bi. Suzy
No comments