BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI (TSPTB) KUFANYA ZIARA YA KITAALUMA KATIKA MIKOA 10
Bodi
ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (TSPTB) inatarajiwa kufanya ziara ya kitaaluma
katika mikoa takribani kumi kwa lengo la kuzungumza na umma wa wanafunzi wa vyuo
vikuu mbalimbali nchini wanaosomea fani
ya ugavi na ununuzi kwa umma sambamba na mafunzo yatakayofanyika siku ya tarehe
25 februari mwezi huu jijini Dar es
salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi
mtendaji wa Bodi ya wataalam wa ugavi na ununuzi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi alisema
ziara hizo imelenga kuwaelimisha wanafunzi wa fani hiyo juu ya maadili ya ugavi
na ununuzi wa umma,
Alisema
mafunzo hayo yatatolewa kwa viongozi wote pamoja na jumuiya ya wanafunzi wa ununuzi na ugavi ambayo yatawajengea uwezo
wa kuwaandaa kulitumikia Taifa kwa uzalendo watakapomaliza.
Aidha
bwana Mbanyi aliongeza kuwa ufanyaji wa mitihani ya kitaaluma chini ya mtaala
uliothibitishwa na taasisi ya kimataifa pamoja na majukumu ya bodi ya usajili
kwa kuwajengea uwezo wa kuwa na mawazo chanya ili kujenga uchumi wa viwanda
nchini.
Wakati
huo huo bodi hiyo inatarajia kuendesha kongamano la siku moja la vijana ambao wanasomea fani ya ununuzi na ugavi
nchini.
Aliongeza
kuwa sambamba na kongamano hilo pia bodi hiyo inataraji kutembelea vyuo vikuu
mbalimbali nchini vinavyofundisha masomo ya ugavi na kutoa mafunzo na kuvitaja
vyuo hivyo kuwa ni chuo cha usafirishaji (NIT)
kilichopo Dar es salaam, CBE Dodoma
na Mwanza, chuo kikuu cha Jordani na Mzumbe kilichopo Morogoro.
Amevitaja
vyuo vingine kuwa ni chuo cha uhasibu Mwanza,
Mbeya na Mtwara (TIA), St.John, UDOM vilivyopo Dodoma, IAA na Chuo kikuu cha
Arusha, SMMUCO NA Mocu vya Moshi, Green Bird kilichopo Mwanga, RUCU Iringa na
SAUTI kilichopo Mwanza na Mtwara.
No comments