Breaking News

TPDC YATOA UFAFANUZI KUHUSU HATUA ILIYOFIKIWA YA UJENZI WA MRADI WA LNG


    Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Eng. Kapuulya Musomba akitoa ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Mradi wa LNG.




   Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Eng. Kapuulya Musomba (Kulia), kushoto ni  Mkurugenzi wa usafirishaji na usambazji wa gesi asilia, Dk. Wellngton Hudson.


Waandishi wa habari kazini


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu mradi wa kusindika gesi asilia kimiminika (LNG), kufuatia taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la the Guardian la Tarehe 13 Februari, 2017, yenye kichwa cha habari “Tanzania LNG Project Stalls as Uncertainty rises-report”. Tafsiri ya kichwa cha habari inaonesha kwamba mradi umesimama, ama hatma yake haijulikani.

Kichwa hiki cha habari hakina usahihi kwa kuwa mradi unaendelea vema, hatua mbalimbali za utekelezaji zimefikiwa na mipango ya utekelezaji inafahamika. TPDC kama mbia katika mradi huu inapenda kutoa ufafanuzi na kueleza hatua mbalimbali za mradi zilizofikiwa hadi sasa.
 
HATUA ZILIZOFIKIWA HADI SASA
1. Ardhi kwa ajili ya ujenzi wa awali wa mradi imeshapatikana katika
eneo la Likong’o Mkoani Lindi na tayari Wizara ya Ardhi imeshatoa
hati ya umiliki
(title deed).
 
2. Takwimu mbalimbali zinaendelea kukusanywa baharini na nchi kavu
aidha stadi mbalimbali za awali zinaendelea kubaini namba bora ya
ujenzi wa mabomba na mitambo.
 
3. Upembuzi yakinifu wa kihandisi kuhusu uzalishaji na usafirishaji wa gesi hadi nchi kavu umefikia hatua ya kuridhisha. Gesi itasafirishwa kwa mabomba kutoka baharini hadi nchi kavu kwa umbali wa kilometa 80 hadi 200. Gesi itakayotumika katika mradi huu
imeshagunduliwa kwenye vitalu namba 1, 2 na 4.
 
4. Majadiliano ya makubaliano ya namna ya uendelezaji wa mradi
baina ya Serikali na Makampuni ya Mafuta ya Kimataifa
yaliyowekeza katika mkondo wa juu (IOCs) yanaendelea vema.
 
HITIMISHO
1. Hatua za utekelezaji wa mradi zinafahamika.
 
2. Takwimu zinazohitajika kwa ajili ya mradi zinazohitajika kwa
ajili ya mradi zinaendelea kukusanywa
 
3. Stadi mbalimbali za kubaini utekelezaji bora wa mradi
zinaendelea
 
4. Majadiliano baina ya serikali na makampuni ya mafuta ya
kimataifa yanaendelea.
Hivyo basi dhana ya kuona kama hatma ya mradi haijulikani sio
sahihi. TPDC kwa maendeleo ya Taifa.

Imetolewa na
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania


No comments