TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU WA AFYA YA UZAZI KUJADILI VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Mwenyekiti
wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA ), Bi Athanasia Soka akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
siku mbili wa wadau
wa sekta ya afya ya uzazi kujadili
changamoto ya vifo vinavyotokana na utoaji wa mimba zisizotarajiwa jijini dar
es salaam.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya na Tiba mtakatifu Hurbert Kairuki ( HKMU ),
Dk. Pensiens Mapunda akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wasekta ya afya
ya uzazi kuhusu vifo vinavyotokana na mimba zisizotarajiwa jijini dar es
salaam.
Washiriki wa mkutano wakifuatilia mada mbalimbali wa kati wa
mkutano huo
Na
Frank Wandiba
Chama
cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) kimewakutanisha wadau mbalimbali
jijini Dar es salaam ili kujadili suala zima la madhara yatokanayo na mimba
zinazotolewa kwa njia zisizo salama ambazo zimekuwa zikisababisha asilimia
zaidi ya 13 ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini.
Akiwasilisha
mada katika mkutano mapema leo jijini dar es salaam, Mhadhiri mwandamizi wa
maswala ya afya ya uzazi kutoka chuo kikuu cha mtakafu Hubert, Dk. Pasiens Mapunda
alisema takwimu za shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa kila mwaka wanawake
wa kitanzania Milioni moja upata mimba zisizotarajiwa ambapo asilimia 39 huishia
kwenye utoaji mimba.
Alisema
kufatia utoaji huo wa mimba kwa njia zisizo salama na wakati wa kujifungua
umekuwa ukisababisha asilimia 13 hadi 15 ya wanawake kufariki kutokana na kutokwa
damu nyingi.
Dk
Mapunda Ameongeza kuwa changamoto kuwa ambayo imekuwa ikichangia kuwepo kwa
mimba nyingi zisizotarajiwa ni kukidhiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
kama kubakwa na mzazi, ndugu, hivyo kusababisha wahusika kulazimika kutoa mimba
hizo kwa usiri bila kuzingatia usalama katika utoaji wa mimba.
Aidha
Dk Mapunda alisema asilimia 40 ya wanawake hupatwa na matatizo ambayo
yanahitaji matibabu mara baada ya kutoa mimba, kutokana na sheria ya nchi
imekuwa vigumu kwa wanawake kujitokeza katika vituo vya afya mara baada ya utoaji
mimba usio salama na kupelekea wengi wao kupoteza maisha yao.
Alisema
kwa mujibu wa sheria ya Tanzania ambayo inasema imesema kuwa kutoa mimba ni
kosa na atakaeshikwa mimba adhabu yake ni miaka 14 jela, atakayesaidia kutoa
mimba adhabu yake ni miaka 7 jela na miaka mitatu kwa atakayesaidia vifaa.
Dk
Mapunda ameitaja mikoa ambayo imekuwa na changamoto ya matukio y utoaji mimba
zisizotarajiwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2013, mikoa ya kanda ya ziwa inaongoza
kwa matukio 120,857 ikifuatiwa na Nyanda za juu kusini ambayo idadi ya matukio
ya utoji wa mimba zisizotajiwa 68,910.
Alisema
kwa mujibu wa utafiti huo mkoa ambao ulikuwa na idadi ndogo ya utoaji wa mimba
zisizotarajiwa ilikuwa ni Zanzibar ambapo iliripotiwa kuwa na matukio 3714 hivyo
kushauri kuwa ipo haja kwa serikali kuangalia upya suala zima la mimba
zisizotarajiwa kwa wanawake hapa nchini, kimataifa suala hilo tayali
limekubaliwa kisheria.
Mkutano
huo wa siku mbili ambao umejikita katika kuangalia changamoto za afya ya uzazi
umewakutanisha wadau kutoka wizara ya sheria, wizara ya afya, jeshi la polisi
pamoja na wadau wa maswala ya afya na uzazi salama
No comments