TAASISI YA MOYO MUHIMBILI ULINZI WAIMARISHWA, KISA KULAZWA MFANYABIASHARA YUSUPH MANJI .
Hali
ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi
alikokuwa akihojiwa.
Manji
aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa alipelekwa
hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land
Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.
Askari
wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa
mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga walionekana wakiimarisha
ulinzi.
Ilipofika
saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa
kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.
Akiwa
amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu
kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.
Alipoulizwa
kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa
Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za mgonjwa.
Februari
8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya watu 65,
akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu
masuala ya dawa za kulevya.
No comments