Breaking News

WASHINDI WA TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2016 WAKABIDHIWA TIKETI KWENDA AFRIKA KUSINI.

Mratibu wa Tamasha la majimaji selebuka Bi Reinafrida akimkabidhi tikeyi za ndege kwa mshindi wa pili Allen Nyanginywa tayali kwa maandalizi ya safari ya kwenda nchini afrika kusini kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli yatakayofanyika kuanzia 19 mwezi huu jijini johanesburg kushiriki mashindano ya Chem ride for sight 2017.
Mratibu wa Tamasha hilo Bi Reinafrida Rwezaura akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam juu ya msimu wa tatu wa tamasha la majimaji selebuka.Allen Nyanginywa mshindin wa pili wa mbio za km 100 majimaji selebuka mwaka 2016 akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam.
Na Frank Wandiba
Washindi watatu wa mbio za baiskeli katika tamasha la majimaji selebuka kwa mwaka 2016 leo wameagwa rasmi na kuanza maandalizi ya kwenda nchini afrika kusini kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli yatakayofanyika kuanzia 19 mwezi huu jijini johanesburg kushiriki mashindano ya Chem ride for sight 2017.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam, mratibu wa Tamasha hilo Bi Reinafrida Rwezaura amewataja washindi hao kuwa ni Salum Miraji ambae alishinda nafasi ya kwanza, allen Nyanginywa nafasi ya pili na ipyana Mbongela ambae alishika nafasi ya tatu.

Alisema washindi hao watatu ambao walishiriki shindano la mbio za za baiskeli mwaka 2016 za km 100 kutoka mbinga kwenda songea wanataji kuondoka nchi kuelekea nchini afrika kusini kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli za Chem ride for sight 2017.

Bi Rwezaura alisema baada ya kuwaaga washindi hao wapenzi wa tamsha hilo wake tayali kwa ajili ya msimu wa tatu wa tamasha la Majimaji Selebuka mwaka huu 2017 ambalo limeboreshwa zaidi linatarajiwa kuanza tarehe 23 hadi 30 wezi julai 2017  mjini songea.
Alisema tamasha hilo la selebuka limesheheni michezo ya aina mbalimbali ikiwemo mbio za baiskeli km 100, ngoma za asili, mbio fupi na ndefu km42, km21 na km10 kwa watoto chini ya miaka 18 pamoja na midahalo katika shule za  sekondari.
Ameitaja michezo mingine ni maonyesho ya biashara, utalii wa ndani pamoja na Majimaji selebuka mtu kwao na Majimaji selebuka mkabesa Platform.
Alisema lengo la tamasha hilo ambalo linafanyika kila mwaka tangu mwaka 2015 ni kuibua vipaji na kuviendeleza pamoja na kukuza soko la wajasiliamali na wafanyabiashara wa ndani pamoja na kutangaza bidhaa zao kwa lengo la kuzipatia soko bidhaa wanazozalisha soko pamoja na kuwakutanisha kubadilisha mawazo jinsi wanavyoweza kuboresha bidhaa zao pamoja na namna ya kuwafikia wateja wengi zaidi.
Pia alibainisha kuwa tamasha hilo limejikita katika kutangaza vivuto vilivypo mkoani humo kama utalii wa ndani katika mbiga za wanyama luhira game Reserve, Liparamba Game Reserve, Matogoro Mountain forests pamoja na mbambabay beach, Majimaji Memorial Museum.


No comments