SWALI LA TUNDU LISSU LAZUA MVUTANO MAHAKAMANI
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salum Hamdani, kueleza anachofahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar , Salum Jecha ana mamlaka ya kufuta matokeo ya uchaguzi au laa.
Lissu
alihoji hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Thomas Simba, wakati Hamdani alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya
uchochozi inayomkabili Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio.
Mshtakiwa
Lissu aliomba kujiwakilisha mwenyewe mahakamani hivyo baada ya ushahidi
alimuhoji maswali shahidi kulingana na ushahidi wake.
Swali
hilo la Lissu lilimfanya Wakili wa Serikali, Paul Kadushi, kupinga akitaka
shahidi asijibu kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala Katiba.
Kadushi
alidai shahidi hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba.
Akijibu
pingamizi hilo, Lissu alidai halina msingi wowote kwa sababu suala la Serikali
ya Zanzibar ni halali na limeletwa na
upande wa mashtaka wenyewe katika shtaka la pili na la tatu hivyo wakabiliane
nalo.
Wakili
Peter Kibatala alidai mahakamani hapo kuwa shahidi huyo anapaswa kueleza yeye
mwenyewe kama hawezi kulijibu swali hilo na si vinginevyo na kwamba katika
kuandika uamuzi wake mahakama ipende isipende ni lazima itajibu swali hilo.
Hakimu
Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili aliahidi kutoa uamuzi leo
iwapo shahidi aeleze anachokifahamu kuhusu Katiba ya Zanzibar ama la.
Kabla
ya kufikia katika malumbano hayo Lissu alitaka kujua yeye na washtakiwa wenzake
walikula wapi njama na kuchapisha huo uchochezi.
Alihoji
wao watu wanne waliwasiliana vp? kwa maandishi, email ama simu na saa ngapi,
maswali hayo yalijibiwa na shahidi kwamba hafahamu.
Awali
akihojiwa na Wakili Kibatala kuhusu wapi alipata taarifa za kuwapo kwa
mikusanyiko ya watu katika sehemu za kuuzia magazeti , Hamdani alidai alizipata
kwa RCO wa Kinondoni, Temeke na Ilala na kwa upande wa Zanzibar alipata kutoka
kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani
Athumani.
Shahidi
alidai katika Gazeti la Mawio la Januari 14 mpaka 20 kulikuwa na habari yenye
kichwa cha habari Machafuko yaja Zanzibar na kwamba maneno hayo yangeweza
kuleta chuki, uvunjifu wa amani, uchochezi na hofu.
Alidai
baada ya kuona hivyo na kulinua gazeti hilo alifungua jalada la uchunguzi kisha
aliteua wapelelezi ili kuona kama kuna kesi ya jinai na walipoona waliwafikisha
washtakiwa mahakamani.
No comments