MFANYABIASHARA YUSUF MANJI KAACHIWA HURU KWA DHAMANA YA MILIONI 20
Mfanyabiashara
maarufu Yusufu Manji amepata dhamana baada ya kusomewa shtaka moja la kutumia
dawa za kulevya aina ya heroine.
Manji
amesomewa shtaka hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya wakili wake Alex Mgongolwa kuiomba
dhamana na Jamhuri kusema haina pingamizi kwani shtaka hilo linadhaminika.
Hakimu
Cyprian Mkeha amesema Manji atakuwa nje kwa dhamana kwa sharti la kusaini bondi ya dhamana ya Sh10 milioni na awe na
mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh10 milioni.
Amedhaminiwa
na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwassa.Kesi itasikilizwa tena March 16
No comments