IDADI YA WALIOKAMATWA SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA HADI SASA DAR YATAJWA, MWANAFUNZI KINARA ALIETAJA MAJINA YA VIONGOZI NAYE MBARONI
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa kwa jumla
watuhumiwa 349 katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika na dawa za
kulevya
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo wauzaji, wasafirishaji na
watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba wataanza kufikishwa mahakamani siku ya
kesho, huku mmoja akipandishwa kizimbani leo.
Pia
ametoa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo, ambapo
amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye ni mwanafunzi mwenye
umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi na kuwatuhumu kuwa
wanahusika na dawa na dawa za kulevya.
Kuhusu
askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro amesema askari hao
wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za
Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda
Sirro amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa na kwamba
kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na watakuwa mbaroni
wakati wowote.
No comments