Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akisalimiana na Mwenyeji wake,Daluwesh Dume (katikati) kwenye hafla ya sherehe ya Maulid ya Mtume S.A.W iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa umakini sherehe hizo.
Watoto nao hawakuwa nyuma katika shughuli hiyo.
Mawaidha yakiendelea kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamed S.A.W
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kinondoni Mkwajuni,Almasi Saidi,akitoa mawaidha katika sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W katika Mtaa wa Ada Estate wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kinondoni Mkwajuni,Almasi Saidi,Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (katikati) na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa makini sherehe hizo.
Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro,akizungumza katika maulid hiyo ya sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W.Kushoto ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro.
Wananchiwaliohudhuria katika sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro na Muandaaji wa kumbukizi hiyo,Daluwesh Dume.
Kikundi cha Al Farouq kikipiga dufu wakati wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
|
(Picha
zote na elisa shunda)
NA
ELISA SHUNDA,DAR
MEYA
wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewaomba Mashehe na Wazee wa jiji
kumuunga mkono katika shughuli anazofanya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo
katika jiji hili.
Akizungumza wakati wa maulidi ya kusherehekea
kuzaliwa kwa Mtume wao Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam mhe stahiki Meya Isaya mwita alisema jiji la Dar es Salaam bila dua za
waze, mashekh na viongozi wengine wa dini huwezi kuliongoza kutokana na changamoto
zilizopo.
“
Najua changamoto zilizopo katika jiji hili ni nyingi wazee wangu naomba
mnisaidie sana, peke yangu siwezi, dua zenu na ushauri wenu ndio unaweza
kunisaidia mimi kufanya mambo mazuri” na wananchi wakaishi kwenye mazingira
wanayopenda” amesema Meya Isaya.
Leo
hi mimi nikiwa na kiburi kwenu kwa ajili ya madaraka haya ambayo nyie ndio
mlionipa, sitaweza kutatua changamoto hata moja, zipo changamoto nyingi kama miundombinu ya elimu, na nyingine, ambazo zote zinahitaji kupatiwa ufumbuzi,
nawaombeni sana wazee wangu mnipe baraka zenu” aliongeza.
Akizungumzia suala la maadili Meya Isaya
amesema wazazi hawana budi kuwasaidia walimu, serikali na viongozi kwa ajili ya
malezi bora watoto hususani wakiwa shuleni.
Alisema
ni jambo la ajabu na mtihani mkubwa kwa walimu ikiwa mzazi atashindwa kufatilia maendeleo ya mtoto shueleni na badala yake kuwa mstari wa
mbele kumnunulia simu wakati bado yupo masomoni jambo ambalo linachangia kumfanya ashindwe kuzingatia masomo na badala yake kushinda kwenye mitanda ya kijami.
“
Leo hii mzazi unamnunulia mwanao simu wakati unajua kabisa anasoma, huu
si mtihani jamani!, leo hii mzazi unashindwa kufuatilia maendeleo ya mtoto wako
shuleni huu si mtihani jamani!, nawaombeni sana wazazi tusaidiane kulea watoto wetu”
ameongeza Meya Isaya.
Aidha
Meya Isaya amewataka vijana kuacha tabia a kukaa vijiweni badala yake wajikite
kwenye kufanya kazi, huku akiwaaka wazazi kutokufumbia macho vijana wao ambao hawapendi kujishuguisha.
Amesema
vijana waliowengi hawapendi kujishugulisha na badala yake husubiri kile ambacho
wazazi wa hutafuta jambo ambalo humjengea kijana mazingira ya kuanza kutamani kugawana mali kabla ya wazazi hawaja toweka duniai.
“
Wazazi msiwavumilie vijana wenu ambao wanasubiri nyie muende mkatafute wao waje
wale, leo hii nyumbani unakuta baba, au Mama anapishana na kijana wake ambaye
angekuwa anajitegemea mwenyewe, lakini kuendelea kuishi nao nyumbani mnataka
kuwaongezea umasikini” amesema Meya Isaya.
Matokeo
yake, unakuta kijana anasema Baba unakufa lini, wanawaza kugawana mali
ambazo mmetafuta nyinyi, kabla hata bado hamjatoweka duniani, jambo hili jamani
sio mtihani ndugu zangu?, lazima tuwalee watoo wetu kwenye misingi ya kuwaeleza
kwamba dawa ya kupambana na umasikini
kufanya kazi” amesisitiza.
Hata
hivyo Meya Isaya amewaomba wananchi wa jiji la Dar es Salaam kutunza mazingira
ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
|
No comments