WAZIRI : WANASIASA WANAOENEZA TAARIFA ZA UONGO ZA KUWEPO BAA LA NJAA WAKAMATWE
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameonya kuwa watu wakiwemo
wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo za kuwepo kwa baa la njaa, ni kosa na
wachukuliwe hatua ikiwemo kukamatwa.
Masauni
amesema bado kuna watu wanajichukulia mamlaka ambayo sio yao na kueneza uongo
kuwa kuna njaa nchini, hilo ni kosa kwa kuwa kwa kueneza propaganda hiyo
kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
“Hizo
ni propaganda za watu wasioitakia mema nchi hii ….. mtu anapofanya kosa lazima
achukuliwe hatua …… Jeshi la Polisi liangalieni hili,” alisisitiza.
Masauni
alitoa onyo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya jana mkoani
Rukwa ambako Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alimhakikishia kuwa mkoa huo
hauna njaa, bali una ziada ya kutosha.
“Nyie
wenyewe mmemsikia mkuu wa mkoa (Zelothe) amethibitisha kuwa hakuna njaa mkoani
hapa lakini sio hapa tu, pia mikoa ya Mbeya na Songwe wamenithibitishia kuwa
hawana njaa,” alisema Naibu Waziri Masauni na kuongeza: “
Sasa
wapo wanasiasa uchwara wanaeneza propaganda kuna njaa, sio mamlaka yao
kutangaza kuwa kuna njaa, kueneza uongo kama huo ni si sawa kwa kuwa kunaweza
kusababisha uvunjifu wa amani nchini, wanastahili kuchukuliwa hatua ikiwemo
kukamatwa,” alisisitiza.
Awali
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe alimweleza Naibu Waziri Masauni kuwa hali ya
kiusalama katika mkoa huo ni shwari ambapo amani na utulivu umeshamiri kwa kuwa
una chakula cha kutosha.
Chanzo-Habarileo
No comments