WAKUU WA POLICE JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI EAC WAKUTANA KUJADILI HALI YA UHALIFU AFRIKA MASHARIKI.
Wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki EAC leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na matukio ya uhalifu wa mitandao na viashiria vya ugaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai DCI Ramadhani Kingai akimuwakilisha Kamishna Jeneral wa Polisi IGP Camillius Wambura katika mkutano wa 8 ambao umeshirikisha nchi 6 amesema kuwa viongozi hao wamekutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu.
Amesema kuwa, jumuiya hiyo itahakikisha inaweka mikakati ya kupambana na uhalifu uliovuka mipaka ikiwemo usafirishaji binadamu,dawa za kulevya,ugaidi na hualifu wa mitandao pamoja na kubadilisha uzoefu hasa kwa wenzao waliofanikiwa.
"Wakuu wa kijeshi wamekutana kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uhalifu, ugaidi, uhalifu uliovuka mipaka nchi ili kuhakikisha ardhi ya Afrika inakua salama,tutahakikisha tunawashughulikia wahalifu mpaka sasa tupo salama"amesema DCI Kingai
Amesema kuwa, kwa Afrika Mashariki uhalifu mkubwa ni wa mitandaoni na viashiria vya ugaidi, huo ni uhalifu mpya kutumia mitandao, kwani zamani mtu alikua anafika benki na bunduki kwenda kufanya uhalifu wa wizi lakini kwa sasa mtu anatumia simu kufanya uhalifu." Amesema Kingai
"Tulipofikia inabidi tujifunze mbinu mpya za kukabiliana na wahalifu ili kuhakikisha wananchi na nchi inakua salama hasa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kwani mtu anaweza akawa yupo Kenya lakini akaiba pesa kutoka benki ya Tanzania,"
Kadhalika amesema Tanzania ni moja kati ya nchi inayoshirikiana na nchi nyingine ili kuweza kusaidia ardhi ya Afrika Mashariki inakuwa salama ambapo mpaka sasa wamekuwa wakibadilishana taarifa za wahalifu kupitia mtandao na wengine wamekamatwa na kuweza kudhibitiwa.
"Jumuiya yetu ni budi kuimarisha miundombinu ya usalama na kubadilishana taarifa kwani tunatambua changamoto kubwa ni Uhalifu wa mitandaoni na Vishiria vya ugaidi ndiyo shida inayotusumbua hivyo nchi moja haiwezi peke yake kulabiliana lazima kuwepo na mashirikiano na mikakati ya pamoja" amesema DCI Kingai.
No comments