Breaking News

AUTOEXPO AFRICA WAJA NA MAONESHO YA TEKNOLOJIA ZA MAFUTA NA GESI

Na Neema Mpaka, Dar es Salaam
WAWAKILISHI wa mataifa takribani 22 kutoka ndani na nje ya Afrika wapo nchini kwa lengo la kuonesha teknolojia mbalimbali kwenye mnyororo wa sekta za gesi na mafuta kwa mfululizo wa siku tatu kuanzia leo.

Maonesho hayo yanayojulikana kama Oil and Gas Africa 2024, yanayofanyika kwa mara ya nane mfululizo chini ya uratibu wa Auto Expo Afrika kwa kushirikiana na serikali yanafanyika jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa, pamoja na mambo mengine, maonesho hayo yanatarajia kufungua madirisha ya fursa mbalimbali za uwekezaji kwenye eneo la mafuta na gesi, sambamba na kuchagiza hamasa ya watanzania kuanza kuwekeza kwenye maeneo tajwa.
Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo, Mkurugenzi Muhamasishaji wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) James Maziku, alisema maonesho hayo yamekuja wakati mwafaka kutokana na uhitaji mkubwa uliopo kwenye kuongeza tija za kiteknolojia kwenye mnyororo wa thamani kwenye eneo la mafuta na gesi.

"Bado kuna bidhaa nyingi sana zinazohitaji teknolojia za hali ya juu kwenye eneo hili," alisema na kuongeza; "maonesho haya ni njia rafiki na njia rahisi katika kuvutia uwekezaji"

Aidha, Maziku aliwasihi watanzania kushiriki kwa wingi kujifunza teknolojia zilizopo kwa kuzingatia ni fursa ya pekee ambayo upatikanaji wake hauna gharama na tija yake ni kubwa.





 

No comments