Breaking News

WHI YASHINDA TUZO YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU AFRIKA

Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment (WHI) Dokta Fred Msemwa (wa kwanza kushoto) akionesha Tuzo walioshinda ya Nyumba za gharama nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Africa Union for Housing Finance – AUHF) inayo tambuliwa na Umoja wa Afrika, leo Oktoba 23, 2024 jijini Dar es salaam (Picha zote na Noel Rukanga)
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment (WHI) Dkt. Fred Msemwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Tuzo walioshinda ya Nyumba za gharama nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Africa Union for Housing Finance – AUHF) inayo tambuliwa na Umoja wa Afrika. leo Oktoba 23, 2024 jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mauzo wa WHI, bwana Raphael Mwabuponde akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya Tuzo leo Oktoba 23, 2024 jijini Dar es salaam
Afisa Uhusiano na Masoko Mwandamizi wa WHI, bi Maryjane Makawia akifafanua jambo kuhusu mchamkato mzima wa kupata mshindi wa Tuzo hiyo mapema leo leo Oktoba 23, 2024 jijini Dar es salaam.

Dar es salaam: Watumishi Housing Investment (WHI) imetunukiwa tuzo ya Nyumba za Gharama Nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika Afrika Union for Housing Finance (AUHF) inayotambuliwa na Umoja wa Afrika (Africa Union) tuzo hiyo imetolewa katika mkutano mkuu wa AUHF uliofanyika visiwani Zanzibar.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa WHI, Dokta Fred Msemwa amesema tuzo hiyo ya heshima inatambua jukumu la WHI katika kuiwezesha umiliki wa nyumba kwa watu wa kipato cha chini na kati nchini na juhudi zilizofanywa na WHI katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo za nyumba.

"Tuzo hii ni kuonyesha kuwa ia wanatambua juhudi tunazozifanya katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo za Nyumba ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji mnunuzi na ndio Kuu ya kupata ushindi huo,". Alisema Dkt. Msemwa.

Alisema WHI inakuwa taasisi ya kwanza hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kupata tuzo hiyo ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kuwezesha wananchi kupata makazi kwa bei nafuu katika miaka 10 tangu kuanzishwa kwa WHI na tayari wameshajenga nyumba zaidi ya 1000.

Dkt. Msemwa aliongeza kuwa nyumba za WHI zimekuwa zikiuzwa kwa bei nafuu kwa kati ya asilimia 10 hadi 30 ukilingalishwa na nyumba kama hizo kwenye soko, huku bei ya kununua nyumba ikianzia shill mill 38, bei hizo pamoja na njia nafuu za malipo zimewasaidia watanzania wengi kufikia ndoto zao za kumiliki nyumba.

"WHI katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo za nyumba ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji, mnunuzi ambavyo vilitajwa kama sababu kuu za ushindi huu njia hizo zimeleta unafuu mkubwa sana kwa watu wanaotamani kumiliki nyumba". Alisema Dkt. Msemwa

Aidha Dkt. Msemwa aliongeza kuwa tuzo hiyo pia heshma kwa nchi na anampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulahisisha kuwapa Watanzania makazi ya bei nafuu kupitia ujenzi nafuu wa nyumba hizo

No comments