TCRA YATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU MATAPELI WA MITANDAO
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ulaghai kupitia simu za mkononi unaofanywa na matapeli katika kipindi hiki. Kulia ni Afisa Uhusiano wa TCRA, Bi. Mabel Masasi. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Jijini Dar es Salaam.
Fatma
Salum- Maelezo
SERIKALI
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tahadhari kwa watumiaji
wa huduma za mawasiliano nchini kuwa makini na utapeli unaofanywa kupitia simu
za mkononi.
Kauli
hiyo, imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja Mawasiliano kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Semu Mwakyanjala wakati akizungumza
na waandishi wa habari.
Semu
alisema kuwa kuna ongezeko la matapeli wanaoghushi utaratibu wa mawasiliano na
kuwalaghai watu kutuma pesa kwa simu za mkononi hivyo Mamlaka na vyombo vya
usalama vinashughulikia suala hilo.
“Usitekeleze
maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa mawasiliano ya simu hata kama yanatoka kwa
mtu unayemfahamu, mpigie aliyekutumia ujumbe kwa namba nyingine ili
kuthibitisha," alifafanua Semu.
Alitahadharisha
kuwa mtu akipokea taarifa kwa njia ya simu au ujumbe mfupi wa maandishi kuwa
ametumiwa fedha kimakosa na kutakiwa kuzirudisha asifanye hivyo mpaka
atakapojiridhisha na uhalali wa taarifa hiyo.
Akizungumzia
matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mitandao, Semu alibainisha kuwa kwa
miezi miwili ya Novemba na Desemba 2016 jumla ya fedha iliyopita kwenye
mitandao ya simu za mkononi ni shilingi trilioni 13.07 hali inayothibitisha
ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mitandao hapa
nchini.
Alitaja
makampuni yaliyohusika na takwimu za miamala hiyo kuwa ni Zantel (EASY PESA),
Tigo (Tigo Pesa), Vodacom (M PESA), Airtel (Airtel Money) na Halotel
(HALOPESA).
Aidha
aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kuhusu matapeli na kuwasilisha
malalamiko yao ya huduma za mawasiliano kwa TCRA kupitia sanduku la posta 474
Dar es salaam au wafike kwenye ofisi za TCRA zilizo karibu au wapige simu namba
0784 558270, 0784 558271 na barua pepe (malalamiko@tcra.go.tz)
No comments