MSHINDI WA UBUNGE JIMBO LA DIMANI AMEAHIDI KUBEBA KERO ZA WANANCHI ZAO NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI.
Mshindi
wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar Juma Ali Juma
ameahidi kuzibeba kero za wananchi wa jimbo hilo na kuwasilisha serikalini kwa
ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa haraka
Ametoa
ahadi hiyo mara baada ya Msimamizi wa Uchaguzi jimbo hilo, Fatma Gharib Ali
kumtangaza rasmi kuwa mshindi katika uchaguzi huo na kusema kuwa kuwa Ubunge ni
daraja la wananchi na serikali
Uchaguzi
huo mdogo umefanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Hafidh
Ali Tahir akiwa Bungeni Dodoma na umehusisha wagombea kutoka vyama 11 vya
siasa.
Juma
Ali Juma amepata kura 4,860 na kumshinda mpinzani wake kutoka CUF, Abdulrazak
Khatib Ramadhan aliyepata kura 1,234.
Katika
Uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 6, 172 kati ya wapiga kura 9,275
waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura jimboni humo.
Katibu
wa Idara Maalum ya NEC, Itikadi na Uenezi Zanzibar amesema ushindi wa mgombea
wa Chama hicho katika uchaguzi huo umekuwa mkubwa kuliko ule wa uchaguzi wa
mwaka 2015, ishara inayotoa matumaini ya kuwa wananchi wa jimbo hilo
wanaendelea kuiunga mkono CCM.
No comments