RIPOTI YA UMOJA WA WAINJILISHAJI WA KIKRISTO TANZANIA (UWAKITA) RAIS MAGUFULI AMEANZA VIZURI KWA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA NA KUSIMAMIA NIZAMU YA KAZI,
Mwenyekiti
wa umoja wa wainjilishaji wa kikristo Tanzania (UWAKITA)Samsoni Bullengi
akifafanua jambo mbele ya waaandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo mara
baada ya kusomwa kwa ripoti ya tathimini ya mwaka mmoja tangu kuingia
madarakani kwa serikali ya awamu ya tano,
Frank Wandiba Dar es salaam,
Umoja
wa Wainjilisti wa Kikristo Tanzania (UWAKITA),
umetoa ripoti ya mwaka mmoja tangu kuingia madarakani serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe.Rais John Pombe Magufuli.
Akisoma
ripoti hiyo mapema leo kwa niaba ya Umoja wa wainjilisti wa kikristo mjumbe
wa umoja huo bwana Elieza Shonza alisema kwa mujibu wa tathmini ya ripoti inaonyesha
kuwa Rais Magufuli ameanza vizuri katika maeneo mbalimbali kama kuziba mianya
ya rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma nchini.
Alisema
ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa Rais Magufuli pamoja na hatua mbalimbali za
makusudi anazoendelea kuchukua kama nizamu ya kazi, kutetea wanyonge, kukusanya
kodi pia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha
wananchi wa kipato cha chini nao wananufaika na rasilimali zilizopo
nchini.
Aidha
Bw.Shonza aliongeza kuwa pamoja na hatua nzuri ambazo amekuwa hakichuka mhe
magufuli pia ripoti hiyo imebaini kuwepo kwa viashiria vya udini kufatia na
baadhi ya viongozi kutoa kauli na matamko ambayo wamekuwa wakitoa hivyo kuzua
sintofahamu jambo ambalo si jema kama
likiachwa liendelee.
Akitoa
mfano wa kauli ambazo waona zinaweza kusababisha msuguano kwa madhehebu ya
imani tofauti kuwa ni kauli aliyoitoa mkuu wa mkoa wa dar es salaam mhe Paul
makonda wakati akizindua ujenzi wa jingo litakalokuwa ofisi ya makao makuu ya
bakwata nchini ambalo linagharim zaidi ya Bilioni 5.
Alisema
Umoja wa wainjilisti tanzania unamwomba mkuu wa mkoa wa dar es salaam
kujitokeza na kutolea ufafanuzi juu ya fedha ya ujenzi wa Jengo la makao makuu
ya baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), fedha hizo zinatoka katika mfuko
gani hili kuondoa dhana potofu iliyopo kwa watanzania,
Bwana
Shonza aliongeza kuwa kama serikali inagharamia ujenzi huo ieleze uhalali wake
wa kusimamia moja kwa moja ujenzi wa taasisi ya dini hatua ambayo ni kukiuka
katiba ya Jamhuri wa Muungano ibara ya 19.
No comments