RAIS MSTAAFU KIKWETE AKUTANA NA MABILIONEA WAKUBWA DUNIANI
Rais
mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Bill Gates ambaye mpaka January 2017
jina lake limetajwa kuwa ndio anashika namba 1 kwa utajiri duniani
Davos Uswisi.
Rais
wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
amepata nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani
Davos nchini Uswisi.
Dr.
JK ameshiriki katika uzinduzi wa baraza la kutokomeza Malaria Duniani (End
Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 January 2016 huko Davos Uswisi ambapo
baraza la kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri
katika sekta ya umma na sekta binafsi duniani na orodha yenyewe ya Wajumbe ndio
hii hapa chini
1.
Bill Gates – Mwanzilishi na mmiliki wa Bill Gates Foundation
2.
Ray Chambers – Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu
Malaria
3.
Peter Chermin –Mwanzilishi wa Chermin Entertainment na Chermin Group
4.
Aliko Dangote – Rais na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group
5.
Idrisa Deby –Rais wa Chad kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taasisi ya ALMA
6.
Jakaya Kikwete –Rais Mstaafu wa Tanzania
7.
Graca Machel – Mwanzilishi wa Foundation for Community Development,Msumbiji
8.
Luis Alberto Moreno –Rais wa Inter-American Development Bank
9.
Ellen Johnson Sirleaf – Rais wa Liberia.
Jakaya Kikwete na Ray
Chambers
Lengo
la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na
hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030 ambapo
kuanzishwa kwa Baraza hilo kumetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika vita dhidi ya malaria katika miaka 15 iliyopita.
Katika
kikao chake cha kwanza kilichofanyika Davos, Baraza hilo limejadili kuhusu
upatikanaji wa rasilimali za kutosha za kuwezesha kutoa msukumo katika
upatikanaji wa vifaa tiba, dawa, tafiti na uvumbuzi wa mbinu na nyenzo za
kisasa za kuzuia, kupambana na hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Malaria katika
nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.
Akizungumza
mara baada ya uzinduzi wa Baraza hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye
utotoni kwake alipoteza kaka yake kwa ugonjwa wa Malaria pamoja na ndugu
wengine wengi katika maisha yake amesema, ” Kutokomeza Malaria iliwahi kuwa
ndoto isiyotekeleza, lakini sasa kuifikia ndoto hiyo ni dhahiri…..tunawea
kuifanya Malaria kuwa historia na kuutokomeza ugonjwa huu katili katika uso wa
dunia”.
Tanzania
ni moja ya nchi zinazosifika barani Afrika na duniani kwa kuweza kupiga hatua
kubwa katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Katika kipindi cha miaka 10
iliyopita, takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya malaria yamepungua kwa
asilimia 70 na vifo vimepungua kwa asilimia 50.
No comments