PICHA KUTOKA JIMBO LA DIMANI, ZANZIBAR WANANCHI WAPIGA KURA KWA AMANI NA UTULIVU
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu Simai Haji leo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika jimbo la Dimani. (Picha na Aron Msigwa –NEC)
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa tathmini ya hali ya Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika jimbo la Dimani leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa pili ) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya Selemani Hamza (wa Kwanza) akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani kuangalia maendeleo ya Upigaji wa Kura leo.
Picha na 3 na 4 Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.
Baadhi ya Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Kushoto) akizungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo ndani ya kituo cha kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani leo. Wengine wanaochukua taarifa ni Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.

Wananchi wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura katika kituo cha Bweleo katika jimbo la Dimani leo.
Na
Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.
HATIMAYE
wananchi wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika Daftari
la Kudumu la Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga
kura kumchagua Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi cha miaka miaka 4.
Zoezi
la upigaji wa Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1
asubuhi likifanyika kwa hali ya Amani na
Utulivu huku baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza
maandalizi mazuri yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC) kufanikisha
Uchaguzi huo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage
akizungumza kuhusu mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo hilo na kuzungumza
na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo vituoni, Waangalizi wa
Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi huo
amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri
iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura.
“
Viongozi wa Tume tumetembelea vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika jimbo la
Dimani; tumeona wenyewe upigaji wa Kura unaendelea vizuri, tumewauliza
Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi kila mmoja amesema Uchaguzi unakwenda vizuri,
nachoweza kuwaambia watanzania Uchaguzi Dimani unakwenda Vizuri” Amesema Jaji
Kaijage.
Amesema
Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka changamoto
zilizokuwa zikijitokeza katika baadhi ya
vituo vya kupigia Kura.
Ameeleza
kuwa zoezi zima la upigaji wa Kura linaendeshwa kwa uwazi mkubwa, Utulivu na
Amani na kuwawezesha wananchi kupiga kura bila vikwazo vyovyote.
Aidha,
Mhe. Kaijage amebainisha kwamba endapo yatajitokeza malalamiko yoyote wakati
zoezi la upigaji wa Kura likiendelea katika vituo mbalimbali , Mawakala wa
Vyama vya Siasa ambao ni wasimamizi wa Maslahi ya Wagombea na Vyama vyao
Vituoni watajaza fomu ya malalamiko Na. 14 kwa mujibu wa Sheria ambayo inatoa
fursa ya kushughulikiwa kwa malalamiko hayo.
Aidha,
amebainisha kuwa mara baada ya zoezi la upigaji wa kura kumalizika leo saa 10
jioni kazi ya kuhesabu Kura itafuata ili hatimaye wamnanchi wa Jimbo la Dimani
waweze kupatiwa matokeo ya maamuzi waliyoyafanya kupitia Kura zao.
Mhe.
Kaijage amesisitiza kuwa Wasimamizi wote wa Uchaguzi huo wamepewa mafunzo ya
kuzingatia ili kuhakikisha wanaendesha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa na
kuwezesha matokeo kutangazwa kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kumjua mshindi
wa Uchaguzi huo.
“
Endapo taratibu zote za Uchaguzi zitakuwa zimekamilika kwa mujibu wa Sheria,
hakutakuwa na sababu yoyote ya kuchelewesha matokeo,mpaka sasa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi tumeridhishwa na mwenendo mzima wa zoezi la upigaji wa Kura na matokeo
yatatolewa kwa wakati” Amesisitiza.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.
Emmanuel Kawishe akizungumzia zoezi la Upigaji wa Kura amesema kuwa Wapiga Kura
wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliokidhi Sifa na Vigezo vilivyoainishwa
kisheria kuwawezesha kupiga Kura.
Amesema kwa mujibu wa Sheria Msimamizi wa Kituo ndiye
mwenye mamlaka ya maamuzi katika kituo cha kupigia Kura ikiwa ni pamoja na
kuamuru kuondolewa kwa mtu yeyote atakayeonekana kufanya fujo au kuzuia zoezi
la uchaguzi kuendelea kituoni.
Katika
Uchaguzi Uchaguzi huo mdogo wa Ubunge wa jimbo la Dimani jumla ya Wapiga Kura
9,280 wanatarajiwa Kupiga kura katika Vituo 29 huku vyama vya Siasa vyenye
wagombea vinavyoshiriki Uchaguzi huo ni 11 huku Waangalizi wa Uchaguzi
waliojitokeza kushiriki katika Uchaguzi huo ni zaidi ya 300.
No comments