MHE LEMA NA MKEWE WAKANA MASHITAKA DHIDI YAO. MAWAKILI WAKE WAOMBA KESI IPELEKWE MAHAKAMA YA KATIBA
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) jana alikana tuhuma za makosa ya jinai
kwa pamoja na mkewe, Neema, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Mbele
ya Hakimu Mkazi, Nestory Barro, Lema na Neema walikana mashtaka ya kutuma
ujumbe mfupi wa simu ya mkononi wenye matusi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.
Awali
akiwasomea maelezo ya kesi hiyo Wakili wa Serikali Alice Mtenga alidai kuwa
Lema na Neema, Agosti 20 mwaka jana, ndani ya Jiji la Arusha, walimtumia ujumbe
wa simu ya kiganjani kwa mkuu huyo wenye lugha ya matusi, huku wakijua ni kosa
kisheria.
Ilidaiwa
kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka simu namba 0764-150747 kwenda namba 0766-757575
uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”
Baada
ya kuwasomea maelezo hayo ya awali, washtakiwa hao kwa pamoja walikiri kuwa ni
wakazi wa Arusha na Lema ni Mbunge wa Arusha Mjini ila walikataa kusambaza
ujumbe huo wa kumtukana Gambo na tarehe ya kukamatwa kwao.
Hakimu
Barro aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 3, ambapo upande wa Jamhuri utaanza
kuwasilisha ushahidi wake Gambo akiwa wa kwanza.
Baada
ya kesi hiyo kuahirishwa, wakili wa Lema, John Mallya aliiambia mahakama
wanatoa notisi ya kuwasilisha pingamizi la mdomo kwa kuwa hati ya mashtaka ina
mapungufu, na baadaye wataomba mahakama iitupilie mbali hati hiyo.
Hata
hivyo, Hakimu huyo alisema hoja za awali za pingamizi hilo zitasikilizwa
Februari 3 pia.
Mbali
na Mkuu wa Mkoa, Jamhuri inakusudia kuita mashahidi wengine wanne, ilielezwa.
Kwa
mujibu wa Wakili wa Serikali Mtenga upande wake pia utakuwa na vielelezo vitatu
vitakavyotolewa
mahakamani
hapo.
Alisema
mashahidi watano watakaotoa ushahidi wao ni Gambo, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa
Arusha (RCO), George Katabazi, (ASP) Damasi Massawe, mhusika kutoka kampuni ya
simu ya Vodacom pamoja na mtaalamu wa picha.
Pia
alivitaja vielelezo watakavyovitoa katika kesi hiyo kuwa ni nakala ya taarifa
za mawasiliano ya simu kutoka kampuni ya Vodacom, simu ya mshtakiwa mke wa Lema
na taarifa ya uchunguzi kutoka kitengo kinachoshughulikia masuala ya
kiuchunguzi (Forensic Bureau).
Wakati
huo huo, wakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, John Mallya amemuomba
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Bernard Nganga kutoanza kusikiliza
kesi ya kuhamasisha maandamano Septemba Mosi (Ukuta) inayomkabili Lema peke
yake.
Akitoa
ombi hilo jana, Mallya alidai kuwa kesi hiyo ya kuhamasisha maandamano kwa njia
ya mtandao wa kijamii kisha kuusambaza Agosti Mosi hadi Agosti 26 mwaka jana,
haifai kusikilizwa katika mahakama hiyo sababu kuna hoja za Kikatiba.
Alisema
shahidi aliyeandaliwa kwa ajili ya kutoa ushahidi wake ambaye ni RCO, George
Katabazi hapaswi kutoa ushahidi mahakamani hapo, sababu kesi hiyo ina hoja za
kikatiba.
“Mheshimiwa
kesi hii ukiiangalia ipo kikatiba zaidi na kwasababu ipo kikatiba basi sisi
tunaenda Mahakama Kuu ikasikilizwe na majaji watatu ili tupewe tafsiri ya
vifungu vya sheria," alisema Mallya.
Alisema
kwa Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977 inampa haki kiongozi au mwanasiasa kufanya
shughuli za kisiasa.
"Kuwakataza
au kuingilia kati tunataka kujua huko Mahakama Kuu ya Katiba, nani ana mamlaka
ya kuzuia maandamano."
Naye
wakili wa Serikali Mtenga alimuomba hakimu kutupa pingamizi la Mallya
alilolitoa mahakamani hapo, badala yake kesi hiyo iendelee kusikilizwa kwani
upande wa Jamhuri tayari ulishamuandaa
shahidi
wake.
Hakimu
Nganga alisema amesikia hoja za mawakili hao wa pande zote mbili na yeye
anaendelea na kesi hiyo baada ya aliyekuwa
Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augutino Rwezile kupanda cheo na
kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kitengo cha biashara.
Alisema
atatoa uamuzi wa kesi hiyo, kusikilizwa au kwenda kwa majaji watatu Februari 8.
No comments