KUTOKA TABORA: BIBI AKUTWA AMEKUFA HUKU AKIWA NA VIBUYU 5 NA KUKU MWEUPE
Bibi mwenye umri wa miaka 60 amekutwa amekufa
mkoani Tabora huku amevaa nguo nyeusi aina ya kaniki, akiwa na vibuyu vitano na
kuku mweupe, katika mazingira yanayoashiria kushiriki vitendo vya kishirikina.
Aidha,
mwili wa mtu mwingine umekutwa pembeni ya mti aliokuwa akichimba dawa.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis
Selemani iliwataja waliokutwa wamekufa kuwa ni Nsoma Dotto (60) mkazi wa Kijiji
cha Zugimlole Wilaya ya Kaliua na Mayara Marashi (50) ambaye ni mkazi wa
Igunga.
Kamanda
Selemani alisema Nsoma alikutwa akiwa amekufa umbali wa mita 200 kutoka
nyumbani kwake juzi.
Alisema
bibi huyo alikutwa amevaa nguo nyeusi aina ya kaniki akiwa na vibuyu vitano
huku pembeni yake kukiwa na kuku mweupe. Uchunguzi wa awali wa jeshi hilo, unaonesha
kuwa huenda ni imani za kishirikina.
Aidha,
alisema Marashi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwakapinga, Kata ya Nanga,
aliyekuwa mganga wa kienyeji, mwili wake uliokotwa Januari 16, mwaka huu ukiwa
umeanza kuharibika.
Kwa
mujibu wa Kamanda Selemani, mganga huyo wa kienyeji aliondoka nyumbani kwake
Januari 8, mwaka huu kwenda porini kuchimba dawa, lakini hakurudi kijijini hadi
maiti yake ilipookotwa akiwa amekufa.
Alisema
Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho. Aliwaomba wananchi wanaoenda
porini kwa ajili ya shughuli zozote zile, wawe wanatoa taarifa kwa ndugu zao
ili iwe rahisi tatizo linapotokea.
|
No comments