BALOZI SEIF IDDI AZINDUA UVUNAJI MPUNGA WA UMWAGILIAJI WA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA SHADIDI BONDE LA CHEJU KISIWANI UNGUJA
Moja miongoni mwa Ploti za Mpunga uliooteshwa kupitia Mradi wa kuongeza Tija na uzalishaji katika zao la Mpunga Zanzibar kwenye Bonde la Cheju Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Mkulima Rashid Khamis (mwenye kipaza sauti), akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia yake jinsi alivyafaidika na Kilimo cha Mpunga kupitia Mradi wa kuongeza Tija na uzalishaji katika zao la Mpunga Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rasid Mohamed.
Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman kati kati wakijumuika pamoja na Mawaziri, Viongozi wa Serikali, Wakulima na Wananchi katika uzinduzi wa Uvunaji wa Mpunga wa Umwagiliaji Maji kwa kutumia Teknolojia ya Shadidi. Wa kwanza kutoka kulia ni Waziri anayesimamia Tawala za Mikoa Mh. Haji Omar Kheir, Waziri wa Fedha Dr. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moha’d na Waziri wa Kilimo Mh. Hamad Rasid Mohamed. Nyuma ya Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma.
Balozi Seif akimuangalia Mkeke Mama Asha Suleiman akiwajibika katika uvunaji wa zao la mpunga kwenye uzinduzi rasmi wa mpunga wa Umwagiliaji maji kwa kutumia Teknolojia ya Shadidi.
Balozi Seif akizungumza na Viongozi, watendaji wa sekta ya Kilimo, Wananchi na Wakulima katika Bonde la Cheju mara baada ya kuzindua rasmi Uvunaji wa Mpunga wa Umwagiliaji Maji kwa kutumia Teknolojia ya Shadidi.
Balozi Seif akifurahia kazi kubwa inayofanywa na wakulima wa Mpunga katika Bonde la Cheju aliposimamisha ghafla msafara wake kwa lengo la kusaidia ubutaji wa Mpunga kwenye moja ya mashamba yaliyomo ndani ya Bonde la Cheju.

Na Othman Khamis Ame, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi ameiagiza Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar
kuanzisha Duka Maalum litakalohusika na uuzaji wa mchele unaotokana na Mpunga
unaozalishwa na Wakulima pamoja na Taasisi
za Zanzibar.
Alisema hatua hiyo muhimu itawapa
hamasa zaidi Wakulima wa zao hilo
kuongeza juhudi za uzalishaji kupitia Mradi wa kuongeza Tija na uzalishaji wa
Mpunga Zanzibar { ERPP } unaoonekana kuleta mafanikio makubwa ya kipato tokea
kuanzishwa kwake katika kipidi kifupi kilichopita.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo
wakati akizindua rasmi uvunaji wa Mpunga wa Umwagiliaji maji kwa kutumia
Teknolojia ya Shadidi inayosimamiwa na Benki ya Dunia hapo katika bonde la
Mpunga Cheju Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema Zanzibar inaweza kupunguza uagizaji
wa bidhaa za vyakula kama mchele kutoka nje ya nchi kutoka asilimia 80% hadi
40% ifikapo mwaka 2020 iwapo mkazo utaongezwa na wananchi walio wengi Vijijini
wanaojihusisha na Kilimo katika kutekeleza mradi huo.
Balozi Seif aliwaagiza wataalamu wote wa
Sekta ya Kilimo Nchini kuanzia sasa watalazimika kutumia muda wao wa kazi kuwa
karibu zaidi na wakulima ili kufanikisha mradi huo na kuacha tabia ya kubakia
Ofisini.
Alieleza kwamba Kilimo cha mradi wa shadidi
ndio mkombozi pekeeunaoweza kuipunguzia Serikali kutumia fedha nyingi za Kigeni
kwa ajili ya kutumiwa na wafanyabiashara kuagiza bidhaa hiyo nje ya Nchi.
“ Lengo la Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ni kupunguza uagizaji wa bidhaa za vyakula kutoka nje ya nchi kwa
kuongeza uzalishaji mara dufu “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliwashukuru washirika wa Maendeleo wa Kimataifa kwa jitihada zao za kuendelea
kuiunga Mkono Zanzibar katika kuimarisha Miradi ya Maendeleo.
Alisema Zanzibar bado inaendelea kuungwa
Mkono na Washirika mbali mbali wa
Maendeleo Duniani na kuiomba Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na
Uvuvi kuendelea kutafuta washirika wengine wa Maendeleo watakaoweza kusaidia
mipango ya Taasisi hiyo ili kuwaongezea nguvu zaidi za uzalsiahji wakulima wa
Visiwa hivi.
Akisoma Risala kwa niaba ya wakulima wa
Mradi wa Kilimo cha Mpunga wa
umwagiliaji Maji kwa kutumia Teknolojia ya Shadidi Mmoja wa Wakulima hao alisema mradi huo umeleta mafanikio
makubwa yaliyopelekea Robo eka kuvuna kati ya Polo 13 na 14 ikilinganishwa na
kilimo cha zamani walichoambulia Polo 8 hadi 9.
Alisema pamoja na mfanikio hayo alizitaja
changamoto zilizojitokeza katika
harakati zao za kilimo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa usawa wa ardhi katika
mabonde ya Kilimo hicho unaosababisha baadhi ya
ploti kukosa maji ya uhakika ya
kuimarisha kilimo hicho.
Wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
iongeze wawekezaji zaidi watakaoshirikiana nao katika kuimarisha miundombinu itakayosaidia
kufanikisha Mradi huo wa Kuongeza Tija na uzalishaji katika zao la Kilimo.
Mapema Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo
na Uvuvi Mh. Hamad Rashid Mohamed alisema Teknolojia hiyo ya Shadidi ndio pekee
inayoweza kuwakomboa Wakulima wakizingatia kufundishana kwa hatua ya awali ya
kuona.
Mh. Hamad Rashid alisema Hekta 500 pekee ndio zenye miundombinu ya Kilimo cha
Umwagiliaji Maji kati ya Hekta 8,500 za Mabonde yote ya yaliyomo Visiwani Zanzibar.
Alisema
ushirikiano wa pamoja kati ya Viongozi, Wataalamu wa Kilimo, Wananchi na wakulima wenyewe katika kuyatumia vyema mabonde yaliyobakia ya kilimo
kwa kuendeleza Mradi wa Shadidi unaweza kupunguza au kuondosha kabisa uagizaji
wa mchele kutoka nje ya Zanzibar.
Waziri wa Kilimo alifafanua kwamba Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo tayari imeshafanya mazungumzo
ya pamoja na Muwekezaji Mzalendo watakaosimamia ufungaji bora wa Bidhaa za
Zanzibar kwa kutumia nembo maalum ili
ziingie katika soko la Kimataifa kiuhakika.
No comments