TAARIFA WADAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO KUHUSU MWISHO WA KULIPA KWA HIARI
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu imeongeza muda kwa wadaiwa sugu kulipa madeni yao
hadi Desemba 30, 2016.
Hatua ya Bodi inafuatia
mwitikio chanya kutoka kwa wadaiwa ndani ya siku 30 za awali ambazo
zinakamilika leo Desemba 14, 2016.
Akitoa taarifa ya
kuongezwa kwa muda; Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi, Abdul_Razaq Badru amesema kuwa
wadau wameomba kuongezewa muda kutokana na baadhi yao kukabiliana na changamoto
za majukumu ya kazi na hivyo kushindwa kujitokeza ndani ya siku 30 zilizokuwa
zimetangazwa awali.
Katika hatua nyingine,
Bw. Badru amesema kuwa ndani ya siku za nyongeza Ofisi za Bodi ya Mikopo
zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitaendelea kuwa wazi kwa siku za
Jumamosi, Disemba 17, 2016 na Jumapili, Disemba 18, 2016 kuanzia saa 3:00
asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo
ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao kupata taarifa kuhusu
madeni yao na kulipa.
Ili kuharakisha utoaji
wa muhtasari wa deni la mdaiwa; mhusika aje na Majina yake kamili, Chuo
alichosoma, Mwaka wa kuanza na wa kuhitimu, anuani yake ya barua pepe (email),
nambari ya simu ya kiganjani, mwajiri wake na Check Number yake iwapo
ameajiriwa serikalini.
‘Kuwa Mzalendo, Rejesha
Mkopo wa Elimu ya Juu’
Kwa mawasiliano zaidi
piga 0763 459165 au 0767 513208
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA
WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
14/12/2016
No comments