MKUU WA MKOA WA SIMIYU ATINGA GAMBOSHI, ENEO MAARUFU KAMA IKULU YA WACHAWI, AWEKA REKODI YA KUWA KIONGOZI PEKEE WA SERIKALI KUTEMBELEA
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka (Kulia) akiwa ameambatana na Askofu Mkuu Kanisa la Waandventisti Wasabato Jimbo kuu la Kusini Mwa Tanzania Mark Malekana, wakati akiingia katika kijiji maarufu nchini Gamboshi 'Gambosi' kilichopo wilaya ya Bariadi Mkoani humo, ambapo Mtaka amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza nchini kufika katika kijiji hicho tangu kianzishwe.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akiongea na wananchi wa Kijiji maarufu nchini Gamboshi 'Gambosi' kilichopo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa amekuwa kiongozi wa kwanza mkuu ngazi ya Mkoa kufika katika kijiji hicho, ambapo alifika kwa ajili ya kuongoza harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 2013.
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa harambee
Diwani kata ya Gambosi Bahame Kaliwa akizungumza
Askofu Mkuu Kanisa la Waandventisti Wasabato Jimbo kuu la Kusini Mwa Tanzania Mark Malekana, ambaye ni mzaliwa katika kijiji hicho maarufu nchini Gambosi, akiongea na wananchi wa kijiji hicho wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi.
Wakazi wa Gambosi
Askofu Mkuu Kanisa la Waandventisti Wasabao Jimbo kuu la Kusini Mwa Tanzania Mark Malekana, ambaye ni mzaliwa katika kijiji hicho maarufu nchini Gambosi, akiongea na wananchi wa kijiji hicho wakati wa harambee ya kuchagisha ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi.
Kulia ni mzee maarufu katika kijiji cha Gambosi Shabani Masuka, (kushoto) ni Paroko wa parokia ya Ngulyati John Nkinga.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano.
Magari yaliyowashangaza wananchi wa kijiji hicho, ambapo kila mmoja alibaki na mshangao kwa kile kilichoelezwa hakujawahi kufika msafara mkubwa wa magari kama hayo.
"Gambosi"
maarufu Gamboshi ni kijiji kinachopatikana katika wilaya ya Bariadi Mkoani
Simiyu, kabla ya kuundwa kwa mkoa wa Simiyu, awali kilikuwa mkoa wa Shinyanga.
Ni
kilometa zaidi ya 30 kufika katika kijiji hicho kutokea mjini Bariadi.
Gambosi/Gamboshi
ni kijiji kinachofahamika kwa historia kubwa hapa nchini, kinafahamika kama
kijiji cha Wachawi, Ikulu ya wachawi nchini.
Tangu
kuanzishwa kwa kijiji hicho hakuna kiongozi yeyote wa mkoa ambaye amefika
kijijini hapo.
Kutokana
na historia yao ilikuwa vigumu kwa wakuu wa mikoa kufika katika kijiji hicho,
lakini juzi mwanga ulionekana kwao, baada ya mkuu wa mkoa wa Kwanza Antony
Mtaka kufika kijijini hapo.
Ilikuwa
siku njema na maalumu kwa wakazi wa kijiji hicho, ulikuwa ugeni mkubwa kwao, wa
kushangaza machoni mwao, ilikuwa mwanga mkubwa kwao.
Mtaka
alifika kijijini hapo kwa mara ya kwanza, na kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza kufika
kijijini hapo, ambapo alifika kwa ajili ya kuongoza harambee ya ujenzi wa shule
ya sekondari Gambosi ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 2013.
Mtaka
alikuwa ameambatana na Askofu Mkuu wa kanisa la Wasabato jimbo kuu la kusini
mwa Tanzania ambaye ni mzaliwa wa kijijini hapo Mark Malekana, pamoja na
wafanyabiashara wa mjini Bariadi.
“
Leo ni bahati kubwa sana kwa wananchi wa kijiji hiki, haijawahi kutokea kuingia
msafara mkubwa wa magari kama haya, tena kiongozi ni mkuu wa mkoa kuja hapa
Gambosi!! hii ni bahati kubwa sana kwetu, na ni kama maajabu kwetu, kutokana na
historia mbaya iliyotuzunguka” ,walisikika wananchi hao wakiongea.
Katika
harambee hiyo shilingi milioni 21.7 pamoja na vifaa mbalimbali vya ujenzi
ikiwemo saruji mifuko 604, nondo pisi 100, madawati 80, vitabu 18 na mabati 20.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu Anthony amefika katika kijiji cha Gambosi siku chache tu
mwaka 2016 baada ya Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Shinyanga mhashamu
Liberatus Sangu kufika katika kijiji hicho na kuanzisha kanisa.
Chanzo-Simiyu
News blog
No comments