TANZANIA KUCHUNGUZA MADAI YA MALAWI KUWAKAMATA WAPELELEZI WAKE.
Serikali
inafanya uchunguzi kuhusu tuhuma zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Malawi
kuwa vimewakamata ‘mashushu’ nane wa Tanzania wakijaribu kuingia kinyamela
kwenye mgodi wa ‘uranium’.
Taarifa
zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo juzi zimedai kuwa watu hao nane
walikuwa wapelelezi na kwamba walitaka kuingia kwenye mgodi huo kujaribu kuchunguza
kama nchi hiyo inatengeneza ‘nyuklia’ katika eneo la Kayerekera. Ripoti
iliyowekwa kwenye mitandao mbalimbali ya Malawi pia imedai kuwa watu hao
waliingia nchini humo bila kuwa na nyaraka za kusafiria.
Akizungumzia
madai hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.
Augustine Mahiga jana alifanya mahojiano na The Citizen na kueleza kuwa hakuwa
na taarifa hizo lakini atazifuatilia kwa kina na kufanya uchunguzi kwani ni
tuhuma kubwa na nyeti.
“Ndio
ninasikia hilo kwa mara ya kwanza kutoka kwako. Hizi ni tuhuma kubwa,
nitafuatilia kwa kina leo (jana) jioni kwa kuwasiliana na ubalozi wetu wa
Malawi kufahamu kama wanafahamu lolote kuhusu hili,” Dk. Mahiga anakaririwa.
Hata
hivyo, tofauti na ripoti zilizotolewa kwenye vyombo vya habari vya Malawi,
Msemaji Msaidizi wa Polisi wa eneo la Karonga, George Mlewa alikana ripoti hizo
akidai kuwa watu hao nane waliokamatwa wanachukuliwa kama wahamiaji haramu tu.
“Wakati
tunaendelea na uchunguzi wetu kuhusu suala hili, naweza kusema kuwa ripoti hizo
ni uvumi tu,” alisema Mlewa.
Chanzo:
The Citizen
No comments