KUTOKA SONGEA: AFARIKI BAADA YA NYOKA WAKE ALIYEKUWA ANAMFUGA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI HADI KUFA
Picha
kutoka maktaba
DUNIANI
kuna mambo, ndivyo unaweza kusema kutokana na mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa
ya Songea, Denis Komba (26) kufa baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye
mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.
Komba
alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako
alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.
Mashuhuda
wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye
hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya
Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724
AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.
Akisimulia
tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara
kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga
gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka
mkubwa huku amesimamisha kichwa.
Haule
alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka
pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia
kwenye kalavati la maji.
Aliongeza
kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha
pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu
ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.
Alisema
kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na
watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo
watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule
alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake
walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.
Alisema
wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye
alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.
Habari
zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya
kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za
kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na
umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa
Songea.
Alisema
nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi
zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa
nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa
dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha
Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za
serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.
Aidha
katika tukio lingine, mkazi wa kijiji cha Mdunduwalo Joseph Charles (27)
amefariki dunia kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni na Oddo Komba
(34) mkazi wa Mhepai Peramiho baada ya kuhitilafiana wakati wakitoka kunywa
pombe.
Kamanda
huyo wa polisi alisema, tukio hilo limetokea tarehe 26 mwezi huu saa 1 usiku
katika kijiji cha Mtyangimbole kata ya Gumbiro katika halmashauri ya wilaya ya
Madaba wilayani Songea ambapo chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokea njiani
kati yao wakati wakirudi nyumbani kutoka kwenye klabu za pombe ya kienyeji.
NA MUHIDIN AMRI- SONGEA
No comments