MIKOA YA NJOMBE, IRINGA NA MBEYA VINARA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI, WATU MIL 2.1 WAAMBUKIZWA VVU DUNIA 2015
Kutokana
na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kupungua kwa asilimia 50 duniani kote
na kupelekea watu milioni 2.1 tu kuambukizwa Virusi vya Ukimwi katika mwaka
2015,kumeibua matumaini mapya ya kuwa na watu wasio na maambukizi ya virusi vya
Ukimwi ifikapo mwaka 2030.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard
Maboko aliwaambia waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam kuwa, nchini
Tanzania maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nayo yameshuka kwa asilimia 20
ambapo watu 54,000 wameambukizwa virusi hivyo kwa mwaka 2015 pekee.
Dkt.
Maboko alisema, Ukimwi bado ni janga kubwa duniani na taifa kwa ujumla huku
akitaja kundi la wanawake kuwa ndilo lina kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU
huku mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya ukiwa na kiwango cha juu cha maambukizi
hayo kitaifa.
Aidha,
alisema serikali imejiwekea mikakati kuhakikisha kuwa waliogundulika kuwa
wameathirika wanaanzishiwa dawa, kuhimiza matumizi ya mpira wa kiume, kupunguza
maambukizi mapya kwa asilimia 29 na kutoa elimu kwa wanawake wanaojihusisha na
ngono, kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto.
No comments