SAKATA LA SCOPION MTOBOA MACHO: MKE WA ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION AELEZA MAHAKAMANI JINSI MMEWE ALIVYOCHOMWA VISU
Stara
Sudi, mke wa Saidi Mrisho ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jinsi alivyoshtuka
baada ya kupokea simu aliyopiga mumewe kuwa amevamiwa na kuchomwa visu machoni,
mgongoni na tumboni.
Akiongozwa
na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Salum
Njwete (34) maarufu ‘Scropion’, Stara alimueleza Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa
Septemba 6, saa tano usiku akiwa amelala alipokea simu yenye sauti ya mumewe
ikieleza kuwa amevamiwa.
“Aliniambia
mama Nancy nimechomwa visu hata kuona sioni hapa nilipo nipo Buguruni,” alidai
Stara ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa mashtaka.
Alidai
tangu wafunge ndoa na mumewe Oktoba 2015 , Said alikuwa akifanya kazi ya
kinyozi katika saluni ya Rodgers iliyopo Tabata Sanene.
“Baada
ya kuongea na mume wangu, simu ilikatika lakini wakati natafuta nguo nivae simu
ileile ilipiga na nilipopokea sauti ya mtu mwingine iliongea ambaye ndiye
mwenye simu na aliniambia kuwa mume wangu ana hali mbaya hivyo nifanye haraka
niende Hospitali ya Amana,” alidai Stara.
Baada
ya kupata taarifa hizo, alidai alimweleza mtoto wao mkubwa, Abdul Said (12)
kuwa anaelekea Amana. Lakini kabla ya kwenda huko alichukua pikipiki na kwenda
Mabibo Hosteli anakoishi mama mkwe wake kumweleza taarifa hiyo na kwamba
waliambatana hadi Amana.
Alidai
wakiwa njiani, walimjulisha mdogo wa Saidi, Yahaya Kisukari (23) kuwa kaka yako
amepata matatizo ya kuvamiwa na mtu akachomwa visu na yupo Hospitali ya Amana.
“Tulipofika
Amana, tuliruhusiwa kuingia wodini na kumuona mume wangu akiwa amefungwa bandeji
machoni na sehemu nyingine za mwili, huku damu ikivuja sehemu mbalimbali za
mwili. Hata nguo aliyovaa ilikuwa imejaa damu,” aliiambia Mahakama na
kuongeza:“Baada ya kumvua nguo zilizo- kuwa zimetapakaa damu, tulipewa rufaa
kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu na wakati huo ilikuwa imeshafika saa
sita usiku.”
Stara
alidai baada ya kumuona mumewe aliyechomwa visu na mtu aliyemtaja kwa jina la
Scorpion, alikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Buguruni.
“Baada
ya kutoa maelezo Polisi Buguruni na askari kwenda kuchukua maelezo ya mume
wangu Muhimbili, tulikwenda kumkamata mshtakiwa Salum Njwete,” alidai.
Alidai:
“Septemba 8, tulirudi tena Muhimbili na kupewa taarifa na daktari wa macho
aliyemfanyia upasuaji Said kuwa macho yake hayataona tena.” Stara alidai tangu
waoane na mumewe, hajawahi kupata malalamiko yoyote kuwa mwenza wake huyo ni
mwizi.
No comments