Breaking News

TIC YASAINI MAKUBALIANO NA OXFORD BUSINESS GROUP YA UINGEREZA KUFANYA TAFITI NA KUHAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI ZINAZOPATIKANA NCHINI.

 Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Charlse Mwijage akizungumza wakati wa uzinduzi kitabu maalum cha kuanisha fursa mbalimbali zilizopo nchini, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam
 Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic akizungumza katika hafla hiyo.
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charlse Mwijage (katikati) akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari (kulia) akishikama mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic mara baada ya kuaisiana makubaliano ya kiutafiti katika kuanisha fursa mbalimbali zilizopo nchini, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mitutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam. Picha Kwa Hisani Ya Michuzi.

Wizara ya Viwanda na biashara kupitia Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) wameingia makubaliano na Oxford Business Group (OBG) ya Uingereza kwa ajili ya kufanya tafiti ya fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini ili kuandaa kitabu cha ripoti itakayotumika kuzitangaza fursa hizo dunia.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Mhe Charlse Mwijage alisema Oxford Business Group wamebobea katika kufanya utafiti wa kiabiashara duniani hivyo kupitia makubaliano yaliofikiwa leo  watapita nchi nzima kuainisha fursa zilizopo na kuzitafutia wawekezaji.

“Njia bora ya kuwashawishi wawekezaji waje Tanzania kuainisha na kuandika habari  nyingi  juu fulsa tulizonazo hasa kupita majarida makubwa duniani na vyombo mbalimbali vya habari kwa hili kutangaza fursa ambazo zinapatikana nchini kwetu” Alisema Mwijage.

Mhe Mwijage alisema kumekuwepo na idadi kubwa ya wawekezaji kutoka bara la Asia wanaokuja Afrika hivyo ni wakati mwafaka kwa Tanzania kuweka mazingira rafiki kwa lengo la kuwavutia ili wakija wapaone Tanzania kama sehemu iliyo salama kwa ajili ya kuwekeza.

Aidha Mhe Mwijage wametoa rai kwa watafiti hao kujikita zaidi katika kufanya utafiti ambazo Tanzania nchini isingeweza kufanya pindi watakapo kamilisha utafiti huo utangaze fursa hizo duniani ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi ambao watanzania isingewezekana kuwafikia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TIC, Clifford Tandari amemuakikishia waziri kuwa watalaam hao wanao uwezo wa hali ya juu katika kufanya tafiti na kutoa ripoti ambayo watalaamu wetu awawezi pia kupitia mtandao wao unaofahamika ulimwenguni  kote wataunganisha mtandao wa TIC hili kila mtu apate kujionea fursa zilizopatikana hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic  alisema ubia walioingia na kituo cha uwekezaji nchini (TIC), ni kwa manufaa na nchi na wataendesha utafiti huo nchini kwa muda wa miezi minane kwa kuwahojiwa viongozi mbalimbali wanaosimamia sekta ya uwekezaji


No comments