AJIRA MPYA ZAIDI YA 70,000 SERIKALINI ZAANIKWA
- Madaktari, wauguzi, walimu wapeta, Pia sekta viwanda, kilimo
- Baada ya kusitisha ajira za umma kwa takribani miezi tisa, Serikali imesema katika mwaka huu wa bajeti itaajiri watu 71,496 kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu, afya na viwanda.
Hata hivyo, licha ya kutaja idadi ya watumishi wapya wanaotarajiwa kuajiriwa katika mwaka huu wa fedha, Serikali haijaweka bayana ni lini hasa ajira hizo zitaanza kutolewa licha ya kuwa imebaki miezi sita mwaka wa bajeti kumalizika.
Akijibu maswali yaliyoulizwa juu ya lini Serikali itaanza kutoa ajira, baada ya kuzisitisha kwa muda, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Florence Temba, alisema Serikali inatoa fursa za ajira kama ilivyoelezwa katika mpango mwaka wa fedha 2016/17.
Katika majibu hayo aliyoyatoa kwa niaba ya Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, yalibainisha kwamba ajira hizo zitakuwa kwenye sekta ya elimu, afya, kilimo na mifugo.
No comments