WAZIRI LUKUVI, AWATAKA WAPIMAJI ARDHI KUWA WADILIFU ILI KUONDOKANA NA MAKAZI HOLELA NCHINI
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mhe William Lukuvi akikabidhi cheti kwa mwakilishi
wa makampuni kama ishara ya kutambua mchango wao katika kuwezesha mkutano mkuu huo wa kwanza na kongamano la wapimaji,
kushoto kwake ni mkurugezi wa upimaji wa Ramani bw Justo Lyamuya mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Na Frank wandiba.
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi, amesema, asilimia 85
ya Ardhi nchini haijapimwa, hivyo kufanya wakazi katika miji kuendelea kuishi
kwenye makazi holela.
Mhe Lukuvi, aliyasema
hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika
jijini Dar es Salaam leo, kuwataka wataalam hao, kufanyakazi ya upimaji ardhi
kwa uadilifu ili kuondokana na makazi holela nchini.
Alisema, kutokana na sehemu
kubwa ya ardhi kutopimwa, hali hiyo imekuwa chanzo kikubwa kwa serikali
kupoteza mapato ambayo kama yangekusanywa yangesaidia katika shughuli
mbalimbali za maendeleo kwenye jamii
Lukuvi, alisema
kutokana na mazingira hayo serikali imewaagiza wataalamu hao kujipanga na
kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wawe wamepima ardhi yeny ukubwa wa
viwanja zaidi ya 400.
Aidha, Lukuvi alisema nia
ya serikali nikuona inafanikiwa katika miaka 10 ijayo kwa kila mtu ana kuwa na
hati ya kiwanja au shamba lililopimwa
Aliongeza kuwa
wakati umefika wa kuondokana mfumo wa kizamani wa uandaaji wa hati za karatasi
na baadala yake lazima wataalamu watumie mfumo wa kieletroniki katika umimaji
wa ardhi ya wananchi.
Alisema mfumo huo wa kisasa
utasaidia kuzuia wananchi kudhulumiwa ardhi na baadhi ya watu wenye uroho wa
ardhi kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu
Washirki wa
kongamano hilo wakimsikiliza mgeni rasmi mhe William lukuvi (hayupo pichani)
wakati akifungua mkutano mkuu na kongmano la wapimaji ardhi ampema leo jijini Dar
es salaam
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mhe William Lukuvi akitembelea mabanda ya
washiriki wa mkutano huo kujionea vifaa mbalimbali vya kisasa vya upimaji wa ardhi
"Ni
marufuku kwa wapimaji ardhi walioajiriwa na serikali kuwa na kampuni za upimaji
wa ardhi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondokana na mgongano wa
kimasilahi kati yao na kampuni binafsi,"alisema Lukuvi.
Lukuvi alisema wapimaji wa sekta binafsi wamekuwa wakifanya vizuri ukilinganisha na wale ambao wameajiliwa na serikali.
Naye Rais IST, Martins Chodata alisema kuwa wamejipanga vizuri na kuahidi kuwa watashirikiana serikali katika kazi hiyo ya upimaji ardhi.
Alisema, kuwa hawatakubali kushirikiana na baadhi ya wapimaji ardhi ambao wamekosa maadili na wanaosababisha migogoro nchini.
Lukuvi alisema wapimaji wa sekta binafsi wamekuwa wakifanya vizuri ukilinganisha na wale ambao wameajiliwa na serikali.
Naye Rais IST, Martins Chodata alisema kuwa wamejipanga vizuri na kuahidi kuwa watashirikiana serikali katika kazi hiyo ya upimaji ardhi.
Alisema, kuwa hawatakubali kushirikiana na baadhi ya wapimaji ardhi ambao wamekosa maadili na wanaosababisha migogoro nchini.
No comments