TANZANIA KUWA WENYEJI WA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA WAJASILAMALI WADOGO NA WAKUBWA.
![]() |
Mkurugenzi
wa taasisi ya sekta binafsi nchini Bwana Godfrey Simbeye akifafanua jambo
katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar Es
Salaam.
|
Na Frank Wandiba
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa ishirini moja wa kimataifa wa wajasilia mali wadogo na wakati unaotarajia kufanyika mnamo mwezi wa 12 tarehe 5 hadi saba mwaka huu.
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa ishirini moja wa kimataifa wa wajasilia mali wadogo na wakati unaotarajia kufanyika mnamo mwezi wa 12 tarehe 5 hadi saba mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar Es Salaam mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sekta
binafsi nchini Godfrey Simbeye amesema kupitia kongamano hilo litakalo
wakutanisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali, litasaidia kuitangaza nchi
kimataifa.
Pia
alisema mkutano huo ambao kwa mara ya kwanza unafanyika katika ukanda wa afrika
ya mashariki hivyo kuwa wenyeji wa mkutano huo, utaisaidia kuitangaza nchi
kimataifa hasa fursa zilizopo hasa katika hazma ya kufikia nchi ya viwanda na muunga
mkono Rais John Magufuli katika hazma yake ya kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa
viwanda.
Adha
bw Simbeye aliongeza kuwa kupitia
mkutano huo washriki watapata nafasi ya kukuza wigo wa mtandao ya kibiashara hasusani
kwa makampuni ya ndani kwa pamoja na kubadilishana uzoefu, sambamba na
kutangaza bidhaaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Mkutano
huo ambao umeandalia kwa ushirikiano kati ya taasisi ya sekta binafsi nchini
kwa kushirikiana na AICC –JNICC pamoja na taasisi mbalimbali za kiserikali na
binafsi kama wizara ya Viwanda na Biashara, SIDO, TIC, EPZA, ZIPA, TTB NA TAN-TRADE.
No comments