MWAKA MMOJA WA RAIS MAGUFULI, TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA MAPATO YAKUSANYA WASTANI WA TRILIONI 1.1 KILA MWEZI
Novemba
Tano mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi hii.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, Watanzania wameshuhudia mafanikio makubwa katika katika
sekta ya ukusanyaji kodi kupitia vyanzo
mbali mbali vya mapato.
Hatua
hii inatokana na kuwa Rais Magufuli alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna mfanyabiashara
anayekwepa ulipaji kodi na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanadai risiti kwa
kila bidhaa au huduma wanayolipia.
Hivyo
Serikali hii tangu ianze kazi rasmi imekuwa ikitilia mkazo ukusanyaji wa mapato
ya Serikali kwa kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili
kuongeza makusanyo ya Serikali.
Juhudi
hizi za Rais Magufuli za kuongeza mapato na kudhibiti upotevu wa mapato ya
Serikali zimejionyesha katika mikutano yake mingi ambapo mara nyingi amekuwa
akisema “Ukinunua bidhaa dai risiti na ukiuza bidhaa toa risiti”.
Jitihada
hizo za wa ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali kwa
manufaa zitatekelezwa na uongozi wa Rais Magufuli zinaunga mkono wosia aliwahi
kuutoa Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo alisema kuwa
“Serikali yeyote isiyokusanya kodi ni “corrupt”.
Hatua
hiyo ya kutoa na kudai risiti ina mchango mkubwa kwa serikali katika kukusanya
kodi ambazo zitasaidia katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya,
maji, umeme, usafirishaji, ujenzi na uendeshaji wa serikali kwa ujumla kutokana
na mapato yanayopatikana.
Hapa
nchini, Mamlaka ya Mapato (TRA) ndicho chombo chenye jukumu la kusimamia
ukusanyaji wa mapato ya Taifa na imekuwa ikitimiza lengo hilo kwa kutekeleza
mikakati mbalimbali kama ilivyoainishwa katika mpango mkuu wa miaka mitano.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo, katika kipindi cha mwaka
mmoja wa utawala wa Rais Magufuli kumekuwepo na ongezeko la makusanyo ya mapato
ya serikali yatokanayo na kodi.
Anasema
kuwa katika kipindi hiki, TRA inakusanya
wastani wa trillion 1.1 kila mwezi kuanzia mwezi Novemba, 2015 hadi Septemba
2016.
“Hili
ni ongezeko la asilimia 28.1 kutoka kwenye kukusanya wastani wa shilingi
bilioni 867 kwa mwezi katika kipindi cha mwezi Novemba, 2014 hadi Septemba
2015” anasema Bw. Kayombo.
Makusanyo
ya mapato katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli kuanzia mwezi Novemba
2015 yamekuwa yakiongezeka ikilinganishwa na miaka iliyotangulia kwa mfano
mwaka wa fedha 2015/2016 mapato yaliyokusanywa yalikuwa shillingi trilioni 12.5
ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.4 ya makusanyo ya mwaka 2014/2015.
Aidha
TRA imekwisha kusanya kodi kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwezi
Septemba 2016, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.4 ikilinganishwa na kipindi
kama hiki cha robo mwaka 2015/16.
Bw.
Kayombo anaongeza kuwa kwa sasa TRA inatekeleza mpango mkakati wa nne
wa ukusanyaji kodi wenye dhamira ya kuongeza makusanyo ya kodi za ndani kwa
kuongeza ulipaji kodi wa hiari.
“Jitihada
mojawapo zinazofanywa na TRA ni pamoja na kuboresha mifumo ya makusanyo
inayoendana na mazingira ya sasa ya ukuaji wa teknolojia ili kuhakikisha walipa kodi wanalipa kwa urahisi kama ilivyo
dhamira yake ya kurahisisha ulipaji kodi na kufanya mazingira yawe bora” anasema
Bw. Kayombo.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja ambao Rais Magufuli amekuwa madarakani, juhudi mbalimbali
zimefanyika ili kuhakikisha matarajio ya Rais ya kuimarisha makusanyo ya kodi
na kudhibiti mianya ya rushwa yanafanikiwa.
Mafanikio
hayo yatamuwezesha Rais Magufuli kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa
kampeni zikiwemo kuboresha afya, upatikanaji wa maji, umeme, kutoa elimu bure,
ujenzi wa miundombinu kama vile viwanja vya ndege, reli na barabara.
Aidha
makusanyo hayo yatawezesha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda ambavyo vitatoa
ajira kwa wananchi na serikali kuweza kujitegemea na hivyo kupunguza utegemezi
wa misaada kutoka kwa wafadhili.
Bw.Kayombo
anataja kiini cha ongezeko la kukusanya kodi kuwa ni matumizi ya mashine za
kielektroniki (EFD) ambazo zinatumika zaidi badala ya stakabadhi zinazoandikwa
kwa mkono.
“Matumizi
ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono hayakuwa na ubora mzuri wa kukusanya na
kuongeza mapato na kutunza kumbukumbu sahihi ambayo yaliifanya serikali ipoteze
mapato mengi” anaongeza.
Katika
hatua nyingine TRA ilitoa mashine za EFDs 130 bure kwa makatibu wakuu wa Wizara
mbali mbali kwa ajili ya taasisi za serikali ambazo zinakusanya maduhuli ya
serikali kwa nia ya kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.
Katika
kuhakikisha makusanyo ya kodi
yanaongezeka TRA imeendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi, kufichua wakwepa
kodi, kupambana na rushwa na kupanua wigo wa kodi kwa kusajili wafanyabiashara
ambao hawajasajiliwa sambamba na kuendesha zoezi la kuhakiki namba ya
utambulisho wa mlipa kodi (TIN) linaloendelea jijini Dar es Salaam kwa sasa ili
kuboresha daftari la walipa kodi.
Pamoja
na mafanikio hayo Kayombo alizitaja changamoto wanazokutana nazo katika
ukusanyaji kodi kuwa ni pamoja na taarifa za kodi kutowafikia wananchi wote ili
kujenga uhiari wa kulipa kodi na uwepo wa ukanda mrefu wa Pwani unaosababisha
kuwepo mianya mingi ya ukwepaji kodi ambapo bidhaa huingizwa nchini kwa njia za
panya.
Pamoja
na changamoto hizo, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeendelea kubuni mikakati
mbali mbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuendana na kauli mbiu ya serikali
ya awamu ya tano isemayo “HAPA KAZI TU” ili kutimiza na kuvuka lengo la
kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.
No comments