HUDUMA YA UPANDIKIZWAJI WA VIFAA VYA USIKIVU YAANZA RASMI NCHINI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa
habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa
vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
Mkurugenzi wa kampuni inayotoa huduma na kuuza
vifaa vya usikivu ya Medel Bw. Mohamed Disouky wa kwanza kushoto akimpa maelezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya wa pili kulia jinsi huduma hiyo inavyotolewa wakati wa
uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika
jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
Baadhi ya wazazi wa watoto wenye matatizo ya
usikivu wakiwa katika foleni ya kusubiri huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya
usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa
watoto uliofanyika jijini Dar es salaam.
Na Ally
Daud-MAELEZO
HUDUMA ya upandikizwaji wa
vifaa vya usikivu kwa watoto imeanza kutolewa rasmi nchini katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili baada ya wataalamu wahuduma hiyo kurejea wakitokea mafunzoni nchini
India ili kuweza kusaidia watanzania hususani watoto wenye matatizo ya kusikia.
Akizindua huduma hiyo katika
hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Uisubisya amesema kuwa Huduma hiyo imekua
hadimu nchini hivyo kufanya kugharamia kiasi kikubwa cha fedha kwenda kuwatibia
nje ya nchi.
“Kwakweli huduma hii ya kupandikiza
watoto vifaavya usikivu italeta msaada mkubwa kwa watanzania na kuokoa gharama takribani
shilingi milioni 80 kwa kila motto ambaye alitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi”
alisemaDkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ullisubsya amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa
mstari wa mbele kugundua mapema matatizo ya watoto na kuwaleta katika Hospitali
ya Muhimbili ili wapate taratibu za kupata huduma hiyo bila ya kuchelewa na kupata
madhara makubwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema kuwa Huduma hiyo
ambayo ilikua inafuatwa nje ya nchi sasa inafanyika nchini ikiwa ni jitihada za
serikali katika kuokoa gharama za matibabu nje ya nchi.
AidhaProf.Museru amesema
kuwa hadi kufikia Januari 2017 MNH itaanza kufanya upasuaji na kupandikiza vifaa
vya usikivu ikiwa ni huduma iliyokamilika bila ya kwenda nje ya nchi hivyo kupelekea
kupunguza gharama zaidi na kusogeza huduma karibu.
“Hapa tulipofikia sio mwisho
wa kutoa huduma hii ,tunataka kufikia Januari 2017 tuwe tunafanya upasuaji kabla
ya kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma kamili na tutakuwa tumefikia baadhi
ya malengo tuliyojiwekea mpaka kufikia muda huo” alisema Prof.Museru
AidhaProf.Museru amesema
kuwa Serikali ilianza jitihada za kuile tahuduma hii nchini miaka mitatu iliyopita
kwa kushirikiana na kampuni ya kuuza vifaa vya kupandikiza vifaa vya usikivu ya
Medel kutoka nchini Misri.
Kwa upande wao wazazi wa
motto aliyepandikizwa kifaa cha usikivu Angel Ibrahimu (4) mkaziwa Mbeya
amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa jitihada zake za kufanikisha huduma hiyo kwa
mtoto wake kwani lilikua tatizo ambalo asingeliweza kulitatua kwa uwezo wake.
Katika ufunguzi wa huduma hiyo
ambayo itakua endelevu nchini imepandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 16 hivyo
kuokoa kiasi cha shilingi Mil 300 kama wangeenda nje ya nchi kufata huduma
hiyo, fedha hizo zitapelekwa kusaidia katika utoaji wa huduma nyingine
No comments