ASENGA AMEWASHAURI VIONGOZI NA WATENDAJI, KUACHA KUFANYA KAZI ZAO KWA KUWEKA MBELE ITIKADI ZA VYAMA.
Diwani wa kata ya Tabata mhe Patrick john Asenga amewashauri
viongozi na watendaji wa mitaa wakiwemo mwenyekiti wa mtaa wa msimbazi mama
kuacha kufanya kazi zao kwa kuweka mbele itikadi za vyama pindi wanapotatua
kero za wananchi wa eneo hilo na kusisistiza pia ipo haja ya kutambua mipaka ya
utendaji kazi zao.
Ushauri ameutoa jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea
taarifa kuhusu kusitishwa kwa mkutano wa adhara ambao ulikuwa umepangwa
kufanyika katika kata ya msimbazi mama kufatia uongozi wa serikali ya mtaa huo kupeleka
taarifa alizodai kuwa ni za kuposhaji kwa mkuu wa mkoa dare s salaam na jeshi
la polisi ili kuzuia kufanyika kwa mkutano huo.
Alisema nimepokea taarifa kutoka kwa jeshi la polisi kuwa taarifa
za kiintelejensia zinanyesha kuwa kuna uwezekano wa kutokea fujo katika mkutano
huo pia kutokana na siku hiyo kuwa jumapili jeshi hilo halina na askari wa
kutosha kulinda mkutano huo hivyo kumtaka kusitisha mkutano huo.
Mhe Asenga aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa alizonazo
hatua hiyo ya jeshi la polisi imechukuliwa baada ya viongozi wa mtaa huo kutoa
taarifa za upotoshaji kwa jeshi hilo kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani
hivyo kulitaka jeshi hilo kutokutoa kibali cha mkutano huo.
Akielezea lengo la kufanya mkutano huo mhe asenga alisema
mkutano huo ambao sio wa kiitikadi za kichama kutokana na kutoa mwaliko kwa
watendaji mbali mbalia na hata jeshi la polisi alikuwa na lengo la kukutana na
wanachi wa kata hiyo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za maendeleo
wanazokutana nazo ili kuweza kutafutia ufumbuzi.
Aidha mhe Asenga amewataka wananchi wa mtaa huo kuwa na
subira kwani amekubali na kutii agizo la polisi kutofanya mkutano siku hiyo, ila
ataanza utaratibu mpya wa kuomba kibali kingine cha kufanya mkutano katika eneo
hilo hivyo kuwataka kuendelea kuwa na subira mpaka hapo watakapotangaziwa tena
tarehe ya mkutano mwingine.
No comments