Breaking News

MAUZO YA HISA YASHUKA KWA ASILIMIA 81

                  Afisa Mwandamizi wa masoko wa (DSE) Bi. Mary Kinabo

                                         Na Frank wandiba
MAUZO katika Soko la Hisa Dar es salaam (DSE) yameshuka kwa asilimia 81 kutoka Tsh. Bilioni 9 mpaka kufikia shilingi bilioni 1.7 kutokana na kushuka kwa idadi ya uuzaji wa hisa kufikia shilingi 340,000 kwa wiki hii.

Akitoa taarifa ya kila wiki mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam Afisa Mwandamizi wa masoko wa (DSE) Bi. Mary Kinabo amesema kuwa mauzo hayo yameshuka kutokana na ukubwa wa mtaji wa soko kushuka kwa asilimia 2.79 kutoka trilioni 21.3 kufikia trilioni 20.7.

Amesema ukubwa wa mtaji kutoka makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha shilingi trilioni 8.2 kuma wiki iliyopita.

Aidha Bi. Mary amesema kuwa licha ya idadi ya mauzo kushuka Benki ya CRDB imeshika nafasi ya kwanza katika kuuza na kununua hisa kwa asilimia 53 ikifuatiwa na kampuni ya Bia nchini (TBL) kwa asilimia 35 huku kampuni ya Swissport ikishika nafasi ya tatu ya kununua hisa kwa asilimia 3.

Pia  Bi. Mary ameongeza kuwa licha ya viashiria vya soko kushuka kwa alama 36.6 kutokana na bei za hisa kutoka TBL kushuka kwa silimia 1.08, huku viashiria vya huduma za kibenki na kifedha vikipanda kwa alama 3.64 baada ya mauzo ya DSE kupanda kwa asilimia 11.5.
Share

No comments